Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Prof. John Nkoma akitoa ufafanuzi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, baada ya kufungua mkutano uliowashirikisha viongozi wa TCRA na wamiliki wa Blogs (Bloggers) Tanzania wenye lengo la kutoa mafunzo ya namna ya kutoa taarifa sahihi zisizo na upendeleo hasa wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka ujao. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA)
Mmiliki wa Blog ya Mzee wa Matukio Daima, Francis Godwin, akichangia hoja kuhusu ushirikishwaji wa wamiliki wa blog wa mikoani katika mikutano mbalimbali inayoandaliwa na TCRA. Godwin alichaguliwa katika mkutano huo kuwa mwakilishi wa wamiliki wa blogs wa mikoani katika kamati iliyoundwa katika mkutano huo ya kuhakikisha chama cha mabloga Tanzania kinasajiliwa na kuanza kufanya kazi.
Mmiliki wa Blog ya Bongo Weekend, Khadija Kalili akichangia hoja wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya wamiliki wa blogs wakiwa katika mkutano huo ulioandaliwa na TCRA, jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Assah Mwambene akifunga mkutano huo.
Comments