AFCON 2015:MAKUNDI YA TIMU 16 YATAJWA

Upangaji wa makundi ya timu kumi na sita zilizofuzu kucheza fainali za mashindano ya 30 ya kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2015 yamefanyika katika mji mkuu wa Equatorial Guinea, Malabo.
Mashindano hayo yataanza Januari 17, 2015.Upangaji wa makundi ulirudishwa wiki moja nyuma ili kuiwezesha Equatorial Guinea, kujiandaa baada ya kuchukua nafasi ya Morocco, iliyokuwa iandae mashindano hayo, lakini ilishindwa kufanya hivyo baada ya kutaka mashindano hayo yasogezwe mbele kuhofia ugonjwa wa Ebola ambao umeyakumba baadhi ya mataifa ya Afrika Magharibi, ambako zinatoka timu nyingi zinazoshiriki michuano hiyo.
Mabingwa watetezi Nigeria ni moja ya timu kubwa zilizoshindwa kufuzu kucheza fainali za mwakani, pamoja na Misri na Angola ambazo zote kwa mshangao hazitaweza kushiriki.
Haya hapa makundi manne ya AFCON 2015:
Kundi A Equatorial Guinea, Burkina Faso, Gabon, Congo
Kundi B Zambia, Tunisia, Cape Verde, DR Congo
Kundi C Ghana, Algeria, South Africa, Senegal
Kundi D Ivory Coast, Mali, Cameroon, Guinea
Wenyeji Equatorial Guinea na Congo zitacheza mechi ya ufunguzi wa michuano hiyo. Kundi D ndilo linaloonekana kuwa gumu zaidi kutokana na timu zilizopangwa kundi hilo.CHANZO:BBC

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*