CCM YAPETA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA MBEYA

Na Emanuel Madafa,mbeya

Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mbeya kikiendelea kupata ushindi katika matokeo ya awali katika uchaguzi wa serikali za mitaa huku vyama vya upinzani vikifuata kwa mbali
Kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotelewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya, Mwangi Kundya, yanaonesha kuwa, chama hicho kimefanikiwa kuzoa idadi kubwa ya vijiji hadi sasa.
Akitangaza matokeo hayo mbele ya waandishi wa habariKundya amesema matokeo ya awali katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya lenye mitaa 181, CCM imefanikiwa kupata mitaa 106, Chadema71, NCCR-Mageuzi mmoja.
Wilaya ya Chunya yenye Vijiji 86,ambapo vijiji vilivyokamilisha hesabu ni 74,  CCM ilipata vijiji 67 , Chadema vijiji 7, wakati kwa upande wa vitongoji, CCM ilipata vitongoji 270, huku Chadema ikiambulia vitongoji 18.
Wilaya ya Ileje jumla ya vijiji vyote ni 71 ambapo vijiji 32 vimekamilisha matokeo yake, ambapo CCM imepata vijiji 23, Chadema vijiji 9, ambapo kwa upande wa vitongo….
Wilaya ya Kyela vijiji vyote 93 vimekamilisha matokeo yake, ambapo CCM imepata 79,Chadema 13 , huku uchaguzi wa kijiji kimoja kurudiwa ambapo kwa upande wa vitongoji 469, CCM vitongoji 377, Chadema 88, wakati vitongoji vine uchaguzi kurudiwa.
Wilaya ya Mbarali jumla ya vijiji 102, CCM 81,Chadema 16 ambapo vijiji sita vitafanya uchaguzi wa marudio, ambapo kwa upande wa vitongoji jumla ni 713, ambapo CCM imeshinda vitongoji 570 , Chadema ikiambulia 79 na vitongoji 36 matokeo yake yalikuwa bado.
Wilaya ya Mbozi, vijiji vilivyopo ni 125 ambapo kati ya hivyo 92 matokeo yake yalikuwa tayari ambapo CCM imepata viti 84 na Chadema imepata vijiji nane, huku vijiji 33 matokeo yalikuwa bado, kwa upande wa vitongoji 664, CCM imepata 557 na Chadema 110, CUF viwili,TLP ikiambulia kiti kimoja.
Wilaya Rungwe jumla ya vijiji 155 , CCM imepata 132,Chadema 22, CUF kimoja na vijiji vitano kufanya marudio, wakati upande wa vitongoji vilivyopo ni 694,CCM 578,Chadema 111,CUF 2 na TLP viwili.
Wilaya ya Momba ambayo matokeo yake yamegawanywa katika sehemu mbili kutokana na wilaya kuwa na Halmashauri ya mji wa Tunduma.
Ambapo kwa upande wa vijiji jumla ni 72, CCM imepata vijiji 43,Chadema24 na vijiji vitano kufanyiwa marudio, wakati kwa upande wa vitongoji, jumla ni vitongoji 302, CCM 189, Chadema 53 na vitongoji 60 matokeo yake bado.
Kwa upande wa mitaa katika Halmashauri ya mji wa Tunduma jumla ya mitaa ni 71, CCM imechukua mitaa 25, wakati Chadema imeongoza kwa kupata mitaa 46, hivyo kulazimika kuunda Halmashauri ya mji.
Wakati matokeo ya Wilaya hizo yakipatikana katika mkoa wa Mbeya kwa upande wa Wilaya ya Mbeya Vijijini matokeo ya awali yameshindwa kutolewa kutokana na utata wa hesabu, lakini pia Jografia ya wilaya hiyo kuwa na changamoto ya mpangilio wake.
Hata hivyo, habari za uhakika zinadai kuwa katika uchaguzi wa mamlaka ya mji Mbalizi, CCM imepata vitongoji viwili, huku chadema ikipata vitongoji 10 kati ya 12 hivyo kuwa na uhakika wa kuunda baraza la mamlaka ya mji.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI