MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE AFANYA KAMPENI KATIKA KATA ZA MTANDI NA MWENGE MKOANI LINDI MJINI.

 Baada ya kuhutubia mkutano wa kampeni kwenye Kata ya Mwenge huko Lindi Mjini Mama Salma Kikwete anaonekana akimbeba mtoto Juma Selemani ambaye naye alikuwa miongoni mwa watu waliohudhuria mkutano wa kampeni.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM anayewakilisha wilaya ya Lindi Mjini na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa Kata ya Mtandi katika mkutano uliofanyika katika Mtaa wa Maisara kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa nchini unaotarajiwa kufanyika tarehe 14.12.2014.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM anayewakilisha wilaya ya Lindi Mjini na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa Kata ya Mtandi katika mkutano uliofanyika katika Mtaa wa Maisara kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa nchini unaotarajiwa kufanyika tarehe 14.12.2014.
 Mama Salma Kikwete, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi anayewakilisha Lindi Mjini akishiriki kucheza na baadaye kuwahutubia wananchi wa Kata ya Mwenge huko Lindi Mjini wakati akishiriki kuwapigia kampeni za uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini kote tarehe 14.12.2014.
 Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, CCM, anayewakilisha Lindi Mjini, Mama Salma Kikwete akisalimiana na viongozi wa Kata ya Mtandi iliyoko Lindi Mjini wakati alipotembelea Kata hiyo kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni katika uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini kote tarehe 14.12.2014.
 Mama Salma Kikwete, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi anayewakilisha Lindi Mjini akishiriki kucheza na baadaye kuwahutubia wananchi wa Kata ya Mwenge huko Lindi Mjini wakati akishiriki kuwapigia kampeni za uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini kote tarehe 14.12.2014.John Lukuwi
----
 Na Anna Nkinda – Lindi

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Lindi mjini wametakiwa kutokubali kurubuniwa kwa kitu chochote kile ili wawapigie kura wagombea wa vyama vya upinzani bali  waungane kwa pamoja katika kampeni na kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi wa kishindo.

Mwito huo umetolewa jana na  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete wakati akiwanadi kwa wananchi wagombea wa chama hicho wanaowania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wa Wenyeviti na Wajumbe wa Serikali za Mitaa katika Kata ya Mwenge.
Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema lengo la chama chochote cha Siasa ni kushika Dola kuanzia ngazi ya mtaa  hadi Taifa hivyo  basi wanachama hao wasikubali kurubuniwa bali waendelee kukitetea na kukipigania Chama chao ili kipate  ushindi katika mitaa yote 117 ya Kata hiyo.
“Viongozi wanaogombea tena wamechaguliwa kutokana na kazi yao nzuri. Nanyi ambao kura zeu hazikutosha wakati wa mchakato wa kuchagua msilaumu, bali muwapiganie  wagombea wote na kuhakikisha wanashinda angalieni maslahi ya chama kwanza  mambo binafsi baadaye”, alisema Mama Kikwete.
Aidha Mama Kikwete aliwaomba wananchi wa wilaya hiyo kutumia maarifa na ujuzi waliopewa na Mwenyezi Mungu wa kutambua mema na mabaya na kutokubali kudanganywa na kundi la watu wachache ili waipoteze amani yao.
Mama Kikwete alisema, “Wenzenu wamepiga hatua kubwa za maendeleo  katika mikoa yao huku Lindi Mwenyezi Mungu katupa neema maendeleo yanakuja sasa. Wanakuja huku kuwadanganya ili mfanye vurugu na kurudisha maendeleo yenu nyumba, msifuate mkumbo na kuchezea  amani kwani vurugu zinarudisha nyuma maendeleo”.
Aliwasihi wananchi waliohudhuria mkutano huo kuhakikisha watoto wao wanaenda shule ili wapate viongozi wazuri wa baadaye ambao watawaletea maendeleo kwani bila ya kuwa na elimu ni vigumu kupata maendeleo.
MNEC huyo pia aliwashukuru wanaume waliowaruhusu wake zao kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na kuwapongeza wanawake kwa kutokukubali kubaki nyuma na kuomba kugombea nafasi hizo.
Mama Kikwete yupo wilayani humo kwa ajili ya shughuli za kichama ikiwa ni pamoja na kushiriki kwenye kampeni na kuwanadi wagombea wa chama hicho wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji  utakaofanyika tarehe 14 mwezi huu.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI