Meneja Mauzo wa Serengeti Breweries Ltd Mkoa wa Morogoro
Bw.Moses Bartazary (Mwenye kofia ) akikabidhi Funguo ya Bajaj Limo yenye
uwezo wa kubeba abiria saba kwa mshindi wa kwanza wa shindano la
Tutoke na Serengeti Bi Rukia Almas ambaye ni mkazi wa Kihonda na
mfanyakazi katika Bar ya Kambarage iliyopo manispaa ya Morogoro
Kwa miaka kadhaa, Rukia Almasi, mkazi wa Morogoro amekuwa akizongwa na uvumi kwamba kushiriki promosheni za bahati nasibu ni kupoteza muda, na kwamba ushindi mara nyingi unakua umepangwa. Kwa kutozingatia mawazo na maono hayo ya watu wengi ndiko kuliko mfanya Rukia wa leo kujivunia kumiliki Limo Bajaji ya Serengeti ambayo ina uwezo wa kubeba watu saba kwa mkupuo.
UJASIRI ULIVYO
TENGENEZA MAISHA YA USHINDI KWA MAMA WA NYUMBANI
Kwa miaka kadhaa, Rukia Almasi, mkazi wa Morogoro amekuwa akizongwa na uvumi kwamba kushiriki promosheni za bahati nasibu ni kupoteza muda, na kwamba ushindi mara nyingi unakua umepangwa. Kwa kutozingatia mawazo na maono hayo ya watu wengi ndiko kuliko mfanya Rukia wa leo kujivunia kumiliki Limo Bajaji ya Serengeti ambayo ina uwezo wa kubeba watu saba kwa mkupuo.
Rukia ambaye ndiye mshindi wa kwanza
wa promosheni ya Tutoke na Serengeti mwenye umri wa miaka 41 ni mtalaka na mama
wa nyumbani anayeishi na watoto wake wawili na mtoto wa dada yake huko Kihonda
Morogoro. Tangu atengane na mumewe Rukia anasema aliamua kuhamia Kihonda na kuweka
makazi yake huko kwani gharama ya maisha ni nafuu.
“Baada ya kutengana na mume wangu maisha
hayajawa rahisi. Nilisongwa na huzuni na mara kwa mara nilikuwa nikitafakari mambo
yatakuaje mbeleni, kwa kuwa sikua na kipato maalumu wala kazi ya kudumu”…alisema
Rukia.
Hata hivyo Rukia anasema amekua akijishughulisha
na biashara ndogondogo ili kuweza kuingiza chochote. Wiki iliyopita, Rukia alitangazwa
mshindi wa Limo Bajaji wakati wa droo ya kwanza ya promosheni inayotambulika kama
‘Tutokena Serengeti’.
Akiongelea jinsi gani alivyoibuka
mshindi wa Limo Bajaj Rukia anasema “Kwa jinsi nilivyokuwa nashiriki nilikuwa
kama najaribu vile, siku jihesabia kama na mimi naweza kuwa mshindi…baada ya kuibuka
mshindi nilikuja kugundua kwamba kuishi na ule uvumi wa kwamba ushiriki wa promosheni
hizi ni kupoteza muda, na kwamba ushindi si halali, ilikuwa ni kosa kubwa ambalo
nimewahi kulifanya katika maisha yangu.
“Baada ya kushinda bajaji hii, nina uhakika
kwamba maisha ya familia yangu yatakuwa mazuri kwa sasa, nilichopanga ni
kuitumia kufanya biashara ya usafiri na natumai kipato tutakacho pata kitakidhi
mahitaji mengi muhimu. Shukrani zangu za dhati ziende kwa Serengeti kwa kweli
na napenda kuwahasa watu wote tuchangamkie fursa ambazo zinajileta mbele yetu
kama mimi nilivyofanya kwenye hii ya ‘Tutokena Serengeti,” aliongeza Rukia.
Kwa mara ya kwanza, Rukia alianza kusikia
habari njema kuhusiana na promosheni ya Tutoke na Serengeti kupitia redio akiwa
na wenzake wakipata vinywaji. “Baada ya kusikia tangazo lile, niliamua kwa ujasiri
na kuamini kwamba nitashinda bajaji na punde nilianza kuchukua hatua stahiki.
Niliagiza bia zaidi, chapa ya Serengeti, na kuanza kutuma tarakimu zilizo kuwa chini
ya kizibo kwenda kwenye namba 15317. Nililirudia zoezi hili pindi nilipopata nafasi
ya kufanya hivyo.
Wiki iliyopita, Rukia alikuwa akitazama
TV huku akipata kifungua kinywa na familia yakeambapo namba mpya ikajitokeza katika
kioo cha simu yake huku akipiga hesabu huenda
ikawa simu ya kudaiwa deni. Alipopokea na baada ya salamu, sauti ya kiume
ilisikika ikimpongeza kwa ushindi. “Kwanza sikuamini nikidhani ananitania
lakini nilipoona anasisitiza kwa ujasiri, ndipo nikaamini ni kweli nilikua
nimeshinda. Kwa kweli nilifurahi sana”….alisema Rukia.
Kampeni hii inatoa fursa kwa kila mtanzania
aliye na umri wa miaka 18+ kushiriki na kushinda
zawadi mbalimbali ikiwemo fursa ya kukuza utalii wa ndani kwa kumpeleka mshindi
kufuurahia mapumziko mazuri ya mwisho wa wiki katika hifadhi za taifa, Limo
Bajaj sita za kushindaniwa ambazo zina uwezo wa kubeba abiria saba kwa mkupuo.
Ushindi wa pesa taslim zenye thamani ya milioni 100/= ambazo zimegawanywa
katika makundi y ash. 5000, punguzo la bia sh 300 kwa bia ya Serengeti Premium
Lager na bia za bure ambazo mtu atapewa baa yoyote ile nchini au kwa mawakala.
Ili kufanikisha kampeni hii, kampuni
ya SBL imeungana na B-Pesa, wataalamu wa teknolojia mpya ambayo hivi karibuni walizindua huduma mpya
ya usafirishaji wa fedha ambao watahusika katika kusambaza fedha katika simu za
washindi watakao patikana kokote nchini.
Jinsi ya kushiriki ni rahisi sana
ambapo unachotakiwa kufanya ni kununua bia
ya Serengeti Premium Lager na angalia chini ya kizibo ambapo utaona namba za
kuijiunga kwenye droo na utume kwenda SMS namba 15317. Kumbuka jinsi unavyoshiriki zaidi ndivyo unavyojiongezea
nafasi za kushinda.
Comments