NAIBU WAZIRI WA FEDHA AFUNGUA MKUTANO WA WATAALAMU WA UGAVI ARUSHA

      

unnamed.Naibu Waziri wa Fedha,Adam Malima(kushoto)akisalimiana  na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya  Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB)Ahmed Kilima alipowasili jijini Arusha kufungua mkutano wa Siku mbili wa Wataalamu wa Ugavi nchini,wengine ni kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB,Clemence Tesha na Mwenyekiti wa Bodi hiyo,Dk Hellen Bandio. unnamed1Naibu Waziri wa Fedha,Adam Malima akiongoza na maafisa wa  Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) katika mkutano wa  Siku mbili unaofanyika kwenye kituo cha mikutano cha AICC  jijini Arusha unnamed2Baadhi ya Maafisa Ugavi na Ununuzi wakisoma nyaraka mbalimbali za mkutano huo leo jijini Arusha. unnamed3Naibu Waziri wa Fedha,Adam Malima akisoma hotuba yake kwenye mkutano wa  Siku mbili  wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB)  unaofanyika kwenye kituo cha mikutano cha AICC  jijini Arusha. unnamed4Mkurugenzi Mtendaji wa  Bodi ya  Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB)Clemence  Tesha(kulia)akimpongeza Naibu Waziri wa Fedha,Adam Malima kwa hotuba nzuri. unnamed7Wataalamu wa Ugavi na Ununuzi nchini wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Wazi wa Fedha.
…………………………………………………………………………………….
Mwandishi wetu,Arusha
WIZARA ya Fedha, imeitaka Bodi ya Wataalam wa  Ugavi na Manunuzi nchni  (PSPTB), kutafuta ufumbuzi wa tatizo la kufanya manunuzi bila kuzingatia thamani halisi ya fedha na kuwataka waajiri kuacha mara moja  kuwaajiri watu wasio na sifa kufanya kazi hizo
Naibu Waziri wa Fedha,Adam Malima ametoa kauli hiyo leo  wakati akifungua mkutano wa tano wa mwaka wa Siku mbili unaofanyika kwenye jengo la Mikutano la AICC jijini Arusha ambapo aliwataka Wataalamu hao kuzingatia maadili na miiko ya kazi yao.
Amesema katika bajeti ya mwaka 2014/15 serikali imetega bajeti ya Sh trilioni 20 kati ya hizo asilimia 65 hadi za 70 zinatumika kwenye manunuzi ya bidhaa na huduma mbalimbali,hivyo taaluma hiyo kuwa na umuhimu wa kipee katika kudhibiti mapato ya serikali yasitumike vibaya.
Awali  Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Sr. Dk. Hellen Bandiho, amesema kauli mbiu ya mkutano huo “Thamani halisi ya fedha  za Manunuzi” ikilenga kuhakikisha serikali inapata huduma bora kulingana na fedha inazotumia ili kuinua uchumi wa nchi.
Amesema Bodi hiyo imezalisha wataalam zaidi ya 23,000 katika ngazi mbalimbali ambayo ni sawa na asilimia 47 pekee huku waajiri wengi wakiwa wamewajiri watumishi wasiosajiliwa na Bodi hiyo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA