WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka akizungumza
na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Hyyat Kilimanjaro jijini Dar es
salaam leo kuelezea mambo mbalimbali kuhusu Akaunti ya Escrow.
Baadhi ya wapiga picha wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwajibika kupata picha katika mkutano huo.
…………………………………………………………………………………………………………
WAZIRI
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka amesema
kamwe awezi kujiuzulu wadhifa wake kwa kashfa ya Akaunti ya Tegeta
Escrow iliyomkumba kwani tukio alilolifanya ni la mafanikio makubwa kwa
upande wa shule zake.Alisema kitendo cha yeye kufanikiwa kuomba na
kupokea shilingi zaidi ya bilioni 1.6 kama mchango kwake ni mafanikio
makubwa kwa kufanikisha kupata mchango wa kuendesha shule za Sekondari
ya Wasichana ya Barbro ya Jijini Dar es Salaam pamoja na Shule ya
Wasichana ya Kajumulo ya Mjini Bukoba, hivyo haoni sababu ya kuachia
nyadhifa zake.
Profesa
Anna Tibaijuka ametoa kauli hiyo mapema leo jijini Dar es Salaam
alipokutana na kufanya mazungumzo na waandishi wa habari kuendelea
kutolea ufafanuzi juu ya sakata hilo lililoitingisha Serikali. Hata
hivyo bado anaamini fedha alizopokea ni fedha safi kwani zimetolewa wazi
na kwa nia njema na mchangaji wa fedha hizo.
“…Kama
Serikali itabainisha kuwa fedha hizo ni haramu basi nitazirejesha
Serikalini. Nafanya vitu vingi lakini havionekani na kusisika…naomba
tusiwe watu wa kuhukumu bila kumsikiliza anayetuhumiwa
ni
dhambi tena dhambi ya mauti. Binafsi bado nashangaa kwanini Kamati ya
Zitto (Mwentekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali) haikuniita
kunisikiliza, Kamati ya Zitto kwanini haikuniita kujitetea,” alisema
Prof. Tibaijuka.
Alipoulizwa
haoni fedheha kuandamwa na kashfa hiyo na kwanini asijiuzulu kulinda
heshima yake na wapigakura wake, alisema haoni fedheha yoyote kwake wala
kwa wapiga kura wake. “…Mimi naona ufahari wewe unasema fedheha wewe
vipi…labda fedheha itakuja baada ya kubainika aliyetuchangia fedha hizo
kaziiba.
Akizungumzia
mchango huo wa zaidi ya bilioni 1.6 aliopokea kutoka kwa Mfanyabiashara
James Rugemalira wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits ambao ni
fedha zinazodaiwa kuchotwa kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow, anasema ni
mchango mkubwa ambao hata yeye baada ya kuuona alishtuka na kushukuru
sana kwa mtoaji.
“…Kwa
kweli ulikuwa mchango mkubwa hata mimi nilishtuka pia na kushukuru
sana, baada ya kuuona tulianza kupeana taarifa kuwa kuna neema imetokea.
Hata hivyo si sawa kitendo cha baadhi ya watu na vyombo vya habari
kuwaaminisha wananchi na taifa kuwa tumeiba fedha hizo, ukiangalia
utabaini kuwa hata mimi nimejikuta kwenye mgogoro wa Escrow bila kujua
kutokana na kuhangaika kutafuta fedha za wafadhili kwenye shule yetu.
“…Mimi
ni mbunge lakini sikupewa nafasi ya kujitetea kwenye sakata hili, sasa
tuache kuwaaminisha wananchi propaganda mbaya tena ya uhaini. Uandishi
huu wa kiupotoshaji sio mzuri ni kupotosha jamii. Kimsingi wananchi
wanaitaji taarifa za ukweli na si habari za udaku.” alisema Profesa
Tibaijuka ambaye amegoma kabisa kujiuzulu.
Anasema
kitendo cha wanahabari kuandika kwamba amechota fedha za Escrow ni
upotoshaji kwani yeye hakufanya hivyo. Sasa mi nasema wananchi wangu
ambao wanateseka kule na kilimo alafu wanasikia nimechota fedha za
Escrow wanajisikiaje kwa hili. Kwa hiyo nimekuja hapa kufafanua ili
jambo ili lieleweke kwa kweli mimi kama waziri sihusiki katika miamala
iliyofanyika. “Wanasema ukweli ukidhihiri uongo utajitenga nimeona
kwamba nitoe ufafanuzi.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
Comments