SIMBA YAWASAINISHA WAGANDA WAWILI



seru

Simon Sserunkuma akisaini fomu za Simba
Timu ya Simba imekatisha mkataba na wachezaji wake wawili wakimataifa wote raia wa Burundi, ambao ni Mshambuliaji Hamis Tambwe na Kiungo Pierre Kwizera ikiwa ni siku moja tangu Simba kuifunga Yanga kwenye mchezo wa nani mtani Jembe.
Simba Sports Club imetengua ndoa yake na wachezaji hao wawili wote raia wa Burundi, ili ipate nafasi ya kuwasajili wachezaji wengine wawili wote raia wa Uganda yaani Mshambuliaji Saimon Sserunkuma, na beki Juuko Murushid, na zoezi la kuwasajili limefanikiwa leo.
musheed
Beki Juuko Murushid akisaini mkataba wa kuichezea Simba…
Wachezaji hao Saimon maarufu kama Sam Sserunkuma na Juuko Murushid, waliichezea Simba dhidi ya Yanga jana katika uwanja wa Taifa Jijini Dar-es-salaam, na wote walionesha uwezo mkubwa na kuisaidia Simba kupata ushindi huo wa mabao mawili dhidi ya Yanga.
Baada ya usajili huu sasa wachezaji wakigeni kutoka Uganda wanafikia watano katika klabu hiyo, wakiongozwa na beki George Owino, mshambuliaji Emanuel Okwi, Dan Sserunkuma, Saimon Sserunkuma na Juuko Murushid

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.