UCHAGUZI WA MARUDIO: KATIBU WA MBUNGE AJERUHIWA VIBAYA


Chama cha Demokrasia na Maendeleo wilayani Iringa kimelalamikia rafu na kasoro mbalimbali zilizojitokeza katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Disemba 14 na kusema kuwa uchaguzi huo uligubikwa na kasoro nyingi ambapo wakati uchaguzi huo  wa marudio  ukiendelea hapo jana, watu wasiojulikana wamemshambulia kwa nondo na mapanga katibu wa mbunge wa Iringa mjini Bwana Joseph Mgima.
Akizungumza kwenye mahojiano na mwandishi wetu, Bwana Mgima amesema tukio hilo lilitokea usiku wa juzi majira ya saa Mbili usiku wakati alipokuwa akienda kuzungumza na mawakala wa chama chake kwenye mtaa wa Bwawani kata ya Mkwawa ndipo alipokutana na watu hao waliokuwa kwenye bajaji mbili ambapo mmoja wa watu hao alimpiga teke na kuangukia mtaroni ndipo watu wengine Sita kutoka kwenye hizo bajaji walipoanza kumpiga kwa mapanga.
  
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA wilaya ya Iringa Leonce Marto amesema tukio hilo linauhusiano mkubwa na uchaguzi wa marudio wa wenyeviti na wajumbe katika mitaa 19 katika manispaa ya Iringa akiwatuhumu wapinzani wao wa CCM kutumia mbinu chafu kushinda kwenye mitaa hiyo huku kamanda wa polisi mkoani Iringa Ramadhani Mungi akisema jeshi hilo linachunguza tukio hilo na litawashughulikia wote watakaobainika kufanya uhalifu huo.
  
Zoezi la uchaguzi limefanyika jana ikiwa ni marudio baada ya baadhi ya maeneo katika mitaa ya manispaa ya Iringa kushindwa kufanya uchaguzi huo kutokana na kasoro mbalimbali zilizojitokeza ikiwemo kukosekana kwa baadhi ya vifaa ambapo jumla ya mitaa 10 imerudia kuchagua wenyeviti wa mitaa na wajumbe wao na mitaa mingine 9 imerudia uchaguzi wa wajumbe baada ya wajumbe hao kugoma kwa idadi ya kura.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.