WALIOBADILISHANA WAKE WAFUMANIANA TENA RUNGWE

HATIMAYE wanaume waliobadirishana wake zao wakazi  wa kijiji cha Ndala kata  ya  Kandete,  Halmashauri ya  Busokelo wilayani Rungwe, Mbeya  wafumaniana tena na  mmoja wao kupigwa  faini ya  kulipa    ng’ombe  wawili ikiwa ni fidia ya kukutwa  na mke wa  mtu.

Wanaume hao ambao ni marafiki walioshibana walikuwa wakiibiana wake ambapo kila mmoja alikuwa akichepuka na mke wa mwenzie ambapo juzi walifumaniana wakitoka kwenye korido ya nyumba ya kulala wageni iliyopo kijijini humo.

Ilikuwa patashika nguo kuchanika baada wa watu hao kushikwa na mshangao wakitukea vyumbani huku kila mmoja akiwa amemkumbatia mke wa mwenzie na katika vurumai wasamalia wema waliwapeleka katika serikali ya kijiji.

Baada ya kufika kwenye ofisi ya afisa mtendaji wakajikuta wote wana makosa na ndipo walipoamua kubadirishana wake zao na kuandikishana na kutia sahihi kwenye ofisi hiyo kuwa kila mtu aendeleekuwa na mke wa mwenzie.

Baada ya kufikia muhafaka huo mbele ya afisa mtendaji wa kijiji hicho Anna Lutengano kila mmoja akaelekea nyumbani kwake akiwa na mke wa mwenzake wakiwa wamepeana uhalali wa kuwamiliki.

Siku mbili zilizopita afisa mtendaji huyo alishikwa na butwaa baada ya kuletewa kesi ya watu hao kuwa wamefumaniana tena ambapo Poul Pomboma alifumaniwa akijivinjari na Lusia Luswepo ambaye ni mke wa Ambakisye Mwakasege.

Kwa mujibu wa afisa mtendaji huyo Anna Lutengano ni kuwa kijana Poul wakati wa kubadirishana wake alikuwa bado anaupendo na mke wake na ndiyo maana akaamua kumyemelea na kwenda nae kujivinjari na hatimaye akafumaniwa.

Afisa huyo alisema kuwa baada ya kijana huyo kufumaniwa na mke wa mtu ambaye alikuwa mke wake kabla hawajabadirishana alikiri na kutozwa faini ya kulipa ng’ombe wawili na kulipa faini ya kuendeshea kesi.

Akisimulia mkasa huo mhanga wa tukio hilo Poul Pomboma alisema huenda mwanamke huo  na hawala yake  waliandaa mtego wa fumanizi hiyo kwa lengo la kujipatia kipato na kuwa anajutia kufanya kitendo hicho.

Wananchi kwa  upande wao wamelani   kitendo  hicho na kusema  watakuwa  msitari wa  mbele kupinga  na kukemea  vitendo  hivyo  na kwamba  wanatarajia  kumwandikia  barua  mtendaji wa  kijiji  hicho kwa  lengo la kuwafukuza vijana hao katika kijiji hicho kwa madai kuwa wanawadharirisha.
Mwisho.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*