WAZIRI KAMANI AFUNGUA SEMINA YA VIONGOZI WA WAVUVI WILAYANI UKEREWE


Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Dkt Titus Mlengeya Kamani (Mb) akitoa hotuba ya ufunguzi wa Semina yaViongozi wa Wavuvi (BMU) iliyofanyika Hotel ya Monach Nansio Ukerewe, chiniya udhamini wa mfuko wa Pensheni wa PPF. 
"Ndugu Meneja wa Kanda, napenda kuupongeza Mfuko wa Pensheni wa PPF ambao unatekeleza mojawapo ya sera zake ya kuhakikisha sekta isiyo rasmi inafikiwa kama ilivyo kwa sekta nyingine za uchumi hapa nchini. Hii itaongeza pato la Taifa hivyo kuzidi kuboresha maendeleo ya Watanzania kwa ujumla na kupunguza umaskini. Napenda kuwaambia kuwa kwa kuandaa semina hii muhimu katika eneo ambalo mimi mwenyewe nalisimamia imenipa faraja sana kwa kuona jinsi Mfuko huu wa PPF unavyowajali sekta zote za uchumu wa nchi. Hongereni sana."
Kwa mujibu wa Meneja wa Kanda ya Ziwa Ndugu Meshack Bandawe (pichani aliyesimama) alisifia Mahudhurio ya semina hiyo akisema kuwa yanadhihirisha kuwa kuna mwamko wa jamii ya watanzania kuhusiana na masuala ya hifadhi ya jamii unaendelea kukua na kuimarika

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI