WAZIRI MAKALAAWATAKA WANANCHI KUWAFICHUA WEZI WA MAJI

SAM_0190
Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala akiongea na vyombo vya habaria katika ziara yake ya kikazi jijini hapa kwa lengo la kutembelea miradi ya maji iliyokuwa na changamoto kubwa ya upotevu wa maji inayosababishwa na uchakavu wa miundombinu na wizi wa maji
SAM_0188
 Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala kulia akiwa anasikiliza maelezo kutoka kwa Eng wa maji Bw.Mohamed Ismail katika eneo la chanzo cha maji mto nduruma katikati niKaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji Arusha Eng.Fabian Maganga
SAM_0178
Muonekano wa maporomoko ya maji mto nduruma ni chanzo kikubwa kinachotegemewa Mkoani Arusha katika huduma ya maji
SAM_0191
Askari anayelinda eneo hilo
SAM_0183
Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala wa nne kulia akiwa anateta jambo katika moja ya maporomoko ya maji ijulikanayo kama mto nduruma wengine ni watumishi wa mamlaka hiyo
SAM_0173
Kulia aliyesimama ni Makamu mwenyekiti wa bodi ya maji Mkoa wa Arusha Bw.Joshua Kileo akiwa anazungumza wakati Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala alipokuwa anazungumza na watumishi wa mamlaka ya maji Arusha leo
SAM_0208
Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala akiwa anaangalia moja ya ujenzi wa chanzo kipya cha maji katika eneo la kisongo ambacho kitasaidia wananchi wa eneo hilo kupata huduma ya maji
SAM_0201
Hii ni mitambo ya kuwekea maji dawa
SAM_0200
Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala akiangalia moja ya kisima cha maji katika kijiji cha Olturuto wilaya Arumeru
SAM_0205
Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala akionge akatika moja ya chanzo cha maji kinachotengenezwa eno la kisongo Mkoa Arusha
Na Pamela Mollel wa jamiiblog
Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala amewataka wananchi wa Mkoa wa Arusha kuendelea kuwafichua wale wote wanaoshiriki katika wizi wa maji ili waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria
Alitoa wito huo jana wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi jijini hapa kwa lengo la kutembelea miradi ya maji iliyokuwa na changamoto kubwa ya upotevu wa maji inayosababishwa na uchakavu wa miundombinu na wizi wa maji
Waziri Makala alisema kuwa serikali inafanya jitihada ya kuboresha huduma ya maji ikiwa nipamoja na kuboresha miundombinu,kukomesha wizi wa maji kwa kutoa elimu kwa wananchi
“Wizi wa kujiunganishia maji katika maeneo mbalimbali hapa nchini upo lakini kwa sasa tunaoparesheni ya kuwasaka wale wote wanaotumia maji bila kulipa watambue kuwa kwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria”alisema Makala
Aidha katika moja ya chanzo kikubwa cha maji mto nduruma alisema kuwa chanzo hicho kinategemewa kwa mkoa wa Arusha hivyo alitoa pongezi kwa mamlaka ya maji kwa kuwa wabunifu
Naye Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji Arusha Eng.Fabian Maganga alisema kuwa kwa hivi karibuni walikuwa na zoezi la ukaguzi wa nyumba hadi nyumba na kufanikiwa kuwakamata watu wanaohujumu mamlaka hiyo takribani 750 hivyo zoezi hilo bado ni endelevu

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI