ALIBINO ANASAKWA MWANZA , WATU 15 MBARONI

      

unnamed1AL
.BW. ALFREDY KAPOLE MWENYEKITI WA ALBINO MKOA WA MWANZA AKIZUNGUMZA KATIKA MKOA HUO
unnamed2AL
WAANDISHI WA HABARI SHEILA SEZI NA GRACE CHILONGOLA WALIPOKUWA WAKIONGEA NA MAMA YAKE NA PENDO
unnamed3AL
NYUMBANI KWAO NA MTOTO PENDO, MWENYEKITI WA ALBINO MKOA WAMWANZA ALFREDY NA MWENYEKITI WA CHAWATA MKOA WAKIONGEA NA MAMA PENDO EMMENUEL.
unnamed4AL
SUNGU SUNGU WAKIMSIKILIZA MKUU WA MKOA
unnamed5AL
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA VALENTINO MULOWOLA ALIPOKUWA AKITOA TAARIFA YA UCHUNGUZI HADI SASA
unnamed7AL
MKUU WA MKOA WA MWANZA MAGESA MULONGO AKIZUNGUMZA NA WANANCHI
…………………………………………………………………………………………
Serikali mkoani Mwanza imesema hakuna kulala hadi mtoto Pendo Emmanuel (Albino) apatikane kufatia tukio la kutekwa na watu wasio julikana toka tarehe 27.12.2014 katika kijiji cha Ndami, Tarafa ya Mwamashimba Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza na kisha kutoweka naye kwenda kusiko julikana hadi sasa.
MKUU WA MKOA.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo, alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji hicho katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo na kuwahusisha wananchi wakijiji hicho pamoja na uongozi wa Wilaya na Mkoa huku akitaka kujua hatua iliyofikiwa na wana nchi hao katika kuwabaini walifanya unyama huo.
Mtoto Pendo alitekwa na watu wasiojulikana mnamo usiku wa tarehe 27.12.2014 majira ya saa nne usiku akiwa amelala na wazazi wake huko Nyumbani kwao na kisha watekaji kutoweka naye na kwenda kusiko julikana hadi sasa, huku taarifa za Polisi zikionesha jumla ya watu kumi na watano (15), wakiendelea kushikiliwa na jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Akihutubia wananchi wa kijiji hicho Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, alisema ni tukio la kusikitisha kwani toka mwaka 2007 hakuna tukio la namna hiyo lililo wahi kutokea katika Wilaya hiyo na tukio la mwisho lililotokea lilimkumba mwananchi wa Wilaya hiyo aliyekuwa amesafiri kwenda Mkoani Shinyanga kwa shughuli zake.
Amesema kiburi walicho nacho watekaji hakiwezi kuwa nje ya mipaka ya kijiji hicho cha Ndami bali mpango mzima unajulikana kwa wenyeji na ndio maana ilikuwa rahisi kufanya unyama huo “Kiburi cha watekaji kimo humu humu haiwezekani mtu kutoka mbali aje atekeleze tukio hapa kijijini bila yakuwa na wenyeji lazima kuna mtu au watu walioshirikiana na wahalifu hao”, alisema Mulongo na kuongeza “ kwa mazingira ya Nyumba ya kina Pendo ilipo kule hakuna sehemu yakutokea na kama mliona pikipiki inaranda randa mchana,.. iweje mshindwe kuitilia shaka? Hapana,  hii haikubaliki! mimi nimekuja kuwaambia nataka Pendo apatikane na sio vinginevyo, nawapa siku tano ijumaa nitarudi hapa mniambie Pendo yuko wapi! Alisema mkuu huyo wa Mkoa akionesha kusononeshwa na tukio hilo.
“Mbona mifugo inapo ibwa inapatikana”? Aliwahoji viongozi wa sungu sungu na kusema haiingii akilini kusema wakati wa tukio la utekaji sungu sungu wote walikuwa wamekwenda kula chakula na ndipo kadhia hiyo ilipotokea, mkuu wa mkoa, alihoji kufatia kauli iliyotolewa na kiongozi wa sungu sungu kuwa wakati wa tukio askari wote wa sungu sungu walikuwa wamekwenda kula majira ya saa tatu na tukio kutokea saa nne.
MWENYEKITI WA ALBINO MWANZA.
Awali akielezea kusikitishwa kwake na tukio hilo, Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu wa Ngozi mkoani hapa Alfred Kapole, alisema inasikitisha kuona wanadamu wakiwauwa binadamu wenzao kama vile wanyama bila hata woga na vyombo vya maamuzi vikishindwa kutoa hukumu kwa wakati huku akielekeza lawama zake kwa mahakama na Mkemia Mkuu. “Mh. Mkuu wa mkoa inasikitisha kuona miongoni mwa kesi 72 zilizokuwa mahakamani, ni kesi 3 tu ndizo zilizokwisha kutolewa hukumu” alisema Kapole, na kuongeza ingekuwa ni kesi ya Wabunge wameshindana kwenye masuala ya uchaguzi ingekuwa imekwisha hukumiwa lakini kwakuwa ni mlemavu wa ngozi,   basi kupuuzia kumekuwa kwingi mno. Alisema kapole.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI