BALOZI SEIF ASHIRIKI HARAMBEE CHUO CHA CBE, AKUSANYA MILIONI 540.8

                     

         

 unnamed (50) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd akikabidhi mchango wake wa shilingi milioni 3 kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Mathew Luhanga (katikati) kusaidia uboreshaji wa miundombinu ya chuo hicho jana usiku wakati wa harambee  maalum ya ukusanyaji wa fedha iliyofanyika  Hotel ya Serena jijini Dar es salamm.Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Prof. Emanuel Mjema.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO. unnamed (51)Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd na viongozi wa Chuo cha CBE wakitoa mkono wa shukrani kwa wadau mbalimbali waliotoa michango yao wakati wa harambee ya kuchangia maendeleo ya chuo cha CBE jana usiku jijini Dar es salaam wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho .
unnamed (52)Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd akisoma majumuisho ya michango na ahadi zilizotolewa na wadau mbalimbali waliohudhuria harambee ya kuchangia maendeleo ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) jana usiku jijini Dar es salaam. Kiasi cha shilingi milioni mia tano arobaini, laki nane na elfu ishrini na tisa (540,829,000/=) zikiwa ni ahadi na fedha taslimu zilikusanywa.
unnamed (53)Baadhi ya wadau wa maendeleo wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) wakitoa ahadi na michango mbalimbali kusaidia maendeleo ya chuo hicho jana usiku wakati wa chakula cha hisani cha miaka 50 ya CBE kilichoandaliwa na uongozi wa chuo hicho kusaidia ukusanyaji wa fedha za ujenzi wa miundombinu,vyumba vya mihadhara na madarasa vya chuo hicho.
unnamed (54)Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd na viongozi wa Chuo cha CBE wakitoa mkono wa shukrani kwa wadau mbalimbali waliotoa michango yao wakati wa harambee ya kuchangia maendeleo ya chuo cha CBE jana usiku jijini Dar es salaam wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho .

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI