KIMENUKA CASH MONEY : LIL WAYNE ATISHIA KUMBURUZA BIRDMAN MAHAKAMANI

Lil Wayne X BirdmanHali imeonekana kuwa si shwari katika lebo ya Cash Money, baina ya  Rapa Lil Wayne na baba yake wa hiyari ‘Brayan Adams’ A.K.A Birdman hadi kufikia hatua ya kutaka kuburuzana mahakamani.
Upepo mbaya ulianza kuvuma baada ya Lil Wayne kuanza kulalamika juu ya albamu yake mpya ”The Carter 5′‘ kuzidi kucheleweshwa kutoka, ambapo ilitakiwa iingie rasmi sokoni mwishoni mwa mwaka jana.
Kama hiyo haitoshi, Mapema wiki hii, Weezy aliamua kuwaomba msamaha mashabiki kutokana na kuchelewa kutoka kwa albamu hiyo  kupitia mixtape yake mpya ”Sorry 4 The Wait 2”  ambapo ndani yake amem-diss mtu mzima Birdman kwenye ngoma inayoitwa Coco na kujigamba kwamba yeye ni jeshi la mtu mmoja.
All I got is Young Money, no more Cash nigga,” “Who kept this s**t together? N***a, me, that’s who! Who was there when n***as left? N***a, me that’s who!” Cash Money is an army, I’m a one man army!“.
Hata hivyo Birdman ameendelea kushikilia msimamo wake wa kutotaka kuiachia albamu ya rapa huyo mpaka siku atakayoamua yeye kuitoa na kudai kuwa Weezy bado yupo chini ya mkataba na lebo yake.
Hali iliyompelekea Weezy kuanza kutafuta msaada wa kisheria wa kutaka kuiomba mahakama iweze kumsaidia kutoka katika lebo ya Cash Money na kutokuwa chini ya utawala wa Birdman ambaye ameendelea kuishikilia albamu yake.
Akiamini kuwa bado anamdai Birdman kiasi cha dola milioni 8 kama sehemu ya malipo ya awali kwa ajili ya albamu hiyo huku kukiwepo na tetesi za Rapa huyo kutaka kuhamia katika lebo ya No Limit inayomilikiwa na Master P.
Endelea kutembelea Blogu yako ya kijanja ya Bamiza.com  kwa muendelezo wa habari hii na nyinginezo kibao zinazowahusu mastaa mbalimbali wa hapa bongo na nje.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI