KINANA AAHIDI USHINDI WA KISHINDO KWA CCM ZANZIBAR 2015

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kufyeka majani mbele ya Chuo cha Sayansi ya Bahari (IMS), alipotembelea chuo hicho kilicho chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam eneo la Buyu, Unguja Zanzibar leo wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM pamoja na kusikiliza kero za wananchi ili zipatiwe ufumbuzi. PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Kinana akikagua jengo jipya la Chuo cha Sayansi ya Bahari. Ameahidi mbele ya uongozi wa chuo hicho kuwa ataibana Serikali itoe fedha ilizoahidi kumalizia ujenzi wa chuo hicho ambacho ujenzi wake ulianza mwaka 2004 lakini hadi sasa haujakamilika.
 Kinana akiangalia samaki aina ya kaa akijiandaa kupanda karibu na ufukweni wakati wa ziara yake katika Jimbo la Fueni, Unguja, Zanzibar leo.
 Kinana akipanda samaki aina ya kaa katika ufukwe wa Bahari eneo la Fuoni Zanzibar
 Kinana akikagua shamba la mikoko baada ya kushiriki kuipanda. Aliwasifu wananchi wa Jimbo la Fuoni kwa kuhifadhi mazingira.
 Kinana akipita kwenye mikoko
 Kinana akikata ki kwa kunywa maji ya dafu baada ya kushiriki kupanda samaki aina na kaa na mikoko
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hdhara kwenye Uwanja wa Magereza Kijiji cha Tomondo, Dimani Mkoa wa Magharibi, Zanzibar. Amewahakikishia wana CCM kwamba wajiandae kushinda kwa kishindo katika uchaguzi Mkuu ujao mwaka huu na kuwataka wajenge mshikamano. Pia Kinana aliwataka viongozi kuchagua wagombea wanaopendwa na wananchi si wanaolazimisha kushinga uongozi kwa kutumia fedha.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Magereza, Katika Kijiji cha Tomondo, Wilaya ya Dimani, Mkoa wa Magharibi, ambapo alimtaka Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), ajiuzulu kutoka kwenye Serikali ya Shirikisho baada ya kutofautiana na kuhusu muundo wa muungano ambapo yeye anataka Serikali tatu na wa mkataba, wakati serikjali iliyopo inataka muundo wa sreikali mbili.
 Kinana akisalimiana na wanachama wa CCM alipowasili katika mkutano wa halmashauri ya Wilaya ya Dimani, Mkoa wa Magharibi, Zanzibar. Kulia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi  Ali Idd Seif
 Wasanii wakitumbuiza kwa ngoma wakati Kinana alipowasili kwenye mkutano huo
 Akia mama wakimshamngilia wakati wa mapokezi ya Kinana  katika Ofisi ya CCM Wilaya ya Dimani
 Kinana akikagua kiwanda cha maziwa cha Azam Diary Products Ltd, kilichopo Fumba, Unguja, Zanzibar
 Kinana akiangalia maziwa yanayozalishwa katika kiwanda hicho. Kulia ni Meneja wa kiowanda hicho Kartikumar Dave
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akipakia makasha ya maziwa kwa Folk Lift wakati Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipokwenda kukagua Kiwanda cha maziwa cha Azam kilichopo Fumba, Unguja Zanzibar
 Kinana akizawadia kasha la maziwa
Kinana akikata utepe kuzindua rasmi gari la kubebea wagonjwa lililotolewa na Mbunge wa Jimbo la Fuoni, kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa katika jimbo hilo..
 Wananchi wakishangilia wakati Kinana akihutubia katika mkutano wa hdhara kwenye Uwanja wa Magereza, Kijiji cha Tomondo,

 Ali Aman Abeid Karume akihutubia katika mkutano wa hadhara ambapo aliwashauri wazanzibar kumomba Ali Mohamed Shein kugombea tena urais wa Zanzibar kwa vile katika kipindi cha uongozi wake amefanya makubwa.
 Waziri Kiongozi mstaafu wa Zanzibar, Ali Vuai Nahodha akihutubia katika mkutano huo wa hadhara.
 Mmoja wa akina dada wafuasi wa CCM, akirekodi matukio ya mkutano huku akicheza
 Kinana akihutubia mkutano huo
Baadhi ya wanachama wapya 600 wa CCM wakila kiapo cha utii baada ya kukabidhiwa kadi katika mkutano uliofanyika Uwanja wa Magereza, Zanzibar

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*