KINANA ASEMA WAPINZANI WATAKE WASITAKE KATIBA INAYOPENDEKEZWA ITAPITA KWA KISHINDO

 Wananchi wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipokuwa akiingia kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Tunduni, Jimbo la Uzini, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akiwapungia mkono wananchi alipowasili kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Tunduni, Jimbo la Uzini, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja. PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Kinana akihutubia katika mkutano huo ambapo aliwataka wananchi kuipigia kura ya ndiyo Katiba inayopendekezwa mwaka huu.Kinana aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi Aprili 30, mwaka huu kuipigia kura ya ndiyo Katiba inayopendekezwa ili ipitishwe kwa kura nyingi za kishindo na kuwaacha wapinzani wakisaga meno.
 Katibu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja,Mpambalioto akielezea mbele ya Kinana utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi katika mkoa huo.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai akimpa ndoo yenye zege wakati wa ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kati, Kusini Unguja.
 Kinana akiangalia samaki aina ya Taa alipofika kukagua Soko jipya la samaki eneo la Unguja Kuu Kae Pwani, Jimbo la Koani, Wilaya ya Kati, Kusini Unguja.
 Kinana akikagua Soko hilo la Samaki,
 Mwakilishi wa Jimbo la Chwaka, Issa Haji Gavu akielezea mbele ya Kinana kuhusu utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi katika miradi mbalimbali jimboni humo,
 Kinana akikabidhi jezi kwa mmoja wa manahodha wa timu za soka zilizotolewa kwa Mwakilishi wa Jimbo la Chwaka, Issa Gavu kwa timu mbalimbali katika jimbo hilo.
 Kinana akiangalia miche ya mikarafuu aliposhiriki uatikaji wa miche hiyo katika shamba la Ali's Spice & Fruits, eneo la Kwambani Kijiji cha Kitumba, Jimbo la Koani Zanzibar,

 Kinana akizungumza na Kada wa CCM Salum Suleiman
 Kinana akihutubia wananchi wa Kijiji cha Miwani Jimbo la Uzini, Kusini Unguja, na kujibu kero zao mbalimbali, zikiwemo za ujenzi wa barabara, afya na maji  alizoahidi kuzitafutia ufumbuzi
 Kinana akifungulia maji ya bomba alipokagua kisima cha maji katika Kijiji cha Machui, Jimbo la Koani, Zanzibar
 Kinana akimtwisha ndoo ya maji Riziki Hassan baada ya kukagua mradi wa maji salama katika Kijiji cha Machui, Jimbo la Koani, Kusini Unguja Zanzibar
 Mbunge wa Jimbo la Uzini, Mohamed Seif Mohamed akihutubia katika mkutano wa hadhara ambapo alielezea miradi mbalimbali iliyotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya 2010.
  Mbunge wa Jimbo la Uzini, Mohamed Seif Mohamed akihutubia katika mkutano wa hadhara ambapo alielezea miradi mbalimbali iliyotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya 2010.
 Kinana akimkabidhi Kapteni wa timu ya Wasakatonge, seti ya jezi zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Uzini, Mohamed Seif Khatib kwa ajili ya timu mbalimbali zilizopo katika jimbo hilo.
 Kinana akipandisha Bendera maalumu ya CCM kwa ajili ya kuwaenzi mabalozi wa chama hicho kwa uchapa kazi wao wa kujitolea katika harakati za kuimarisha uhai wa chama katika Jimbo la Uzini.Mkoa wa Kusini Unguja unaongoza kwa kuwa na wanachama wengi nchini.
 Mwakilishi wa wazee wa Wilaya ya Kati, Machano Heri Machano, akimkabidhi Kinana zawadi ya nguo wakati wa mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Tunduni, Jimbo la Uzini.
 Kinana akionesha kadi za wanachama watano wa Chadema waliohamia CCM wakati wa mkutano huo. Kushoto ni mmoja wa akina mama aliyekabidhi kadi hizo kwa niaba ya wenzake.
 Wanachama wapya wa CCM wakipokea kadi kutoka kwa Kinana. Zaidi ya wanachama wapya 400 walijiunga na chama hicho.
Akina mama wakifurahia hotuba ya Kinana katika mkutano huo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.