KINANA ATIMIZA HADI YA SERIKALI KUKIRUDISHA KWA WANANCHI KIWANDA CHA CHAI MPONDE, BUMBURI

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutubia katika mkutano ulioandaliwa rasmi kuwaambia wananchi wa Mponde, Halmashauri ya Wilaya ya Bumburi, Lushoto Tanga, kwamba Rais Jakaya Kikwete amekubali kukirudisha Kiwanda cha Chai cha Mponde kwa wananchi baada ya mgogoro dhidi mwekezaji wa kiwanda hicho, Yusufu Mula uliodumu kwa takribani miaka 10 na kusababisha kiwanda hicho kufungwa maiaka miwili iliyopita na kuwaacha wananchi kwenye lindi kubwa la umasikini.

Hayo ni Mafanikio ya Katibu Mkuu wa CCM,  Abdulrahman. Kinana ambaye katika mkutano wa hadhara uliofanyika Septemba mwaka jana katika Kijiji cha Mponde, aliahidi kupata suluhu ya mgogoro wa kiwanda hicho ulioshindikana kutatuliwa kwa muda mrefu kwa kuupeleka kujadiliwa katika Kamati Kuu ya CCM na kupata ufumbuzi ndani ya mwezi mmoja, ahadi ambayo aliitimiza.

Kiwanda hicho kilifungwa baada ya wananchi kususia kuendelea kulima mashamba ya chai kwa lengo la kuishinikiza Serikali kutatua haraka mgogoro dhidi ya Mwekezaji wa kiwanda hicho, Yusufu Mulla, ambaye walidai kuwa alikuwa anawanyanyasa wakulima wa zao hilo pamoja na wafanyakazi kuwalipa ujira mdogo.

Kinana amesema Serikali itanunua hisa za mwekezaji ili aondoke na kuwaachia wananchi kiwanda hicho.Pia Serikali itatuma jopo la wataalamu watakao tathmini hasara iliyopo, na kutafuta mtaji wa kukifufua kiwanda  ili kianze kufanya kazi.. ;PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ukikata mbuga kuelekea Mponde, Bumburi, L
 Msafara wa Kinana ukiingia kwenye mkutano karibu na Kiwanda cha Mponde
 Kinana akiwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga, Shija Othman akielekea kwenye mkutano kuwapatia wananchi taarifa ya kukirudisha kwa wananchi kiwanda cha Chai Mponde,
 Kinana akilakiwa na wanachi wa Jimbo la Bumburi alipwasili kwenye mkutano huo
 Sehemu ya umati wa wananchi wakiwa kwenye mkutano huo
 Mbunge wa Jimbo la Bumburi, January Makamba akisalimiana na wananchi alipowasili kwenye mkutano huo.
 Mkazi wa Bumburi akiwa amevaa sanamu yenye sura inayofanana na aliyekuwa mmiliki wa Kiwanda cha Chai cha Mponde, Yusufu Mula
 Kinana akifafanua mambo mbalimbali ya jinsi serikali ilivyopanga kukiendesha kiwanda hicho baada ya kukirudisha kwa wananchi.
 Kinana akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Chai TanzaniaMathias Asenga kuelezea hali ya kiwanda hicho ambacho kinatakiwa kufanyiwa matengenezo kidogo  ili kianze kufanya kazi
 Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Wakulima Wadogo wa Chai Tanzania, Mustafa Umande akishukuru uamuzi uliotolewa na Serikali ya CCM wa kukirudhisha kiwanda cha Mponde kwa wananchi na kuwataka wananchi waanze haraka kuandaa mashamba ya chai ili kiwanda kikianza kufanya kazi siku za usoni waanza kuuza chai.
 Baadhi ya wananchi wa Bumburi wakisikiliza kwa makini wakati Kinana akihutubia katika mkutano huo.
 Mbunge wa Jimbo la Bumburi, January Makamba akiishukuru Serikali kwa uamuzi wake wa kukirudisha kiwanda hicho kwa wananchi ambapo pia alimshukuru Rais Jakaya Kiwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman kwa kufanya jitihada za kuhakikisha wananchi wanapata haki yao hiyo walioisotea kwa takribani miaka 10.
Sehemu ya umati wa wananchi waliohudhuria mkutano huo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.