KOMREDI KINANA AHITIMISHA ZIARA PEMBA KWA MAFANIKIO

 Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Abdulrahman Kinana, akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye mkutano wa hadhara kwenye kiwanja cha mpira cha Mjimbini, Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Kinana amemaliza ziara ya siku 15 katika visiwa vya Unguja na Pemba Zanzibar ambapo amekagua na kushiriki ujenzi katika miradi 40 mikoa 12.

Komredi Kinana alijionea mafanikio makubwa ya kimaendeleo yaliyofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais Dk. Ali Mohamed Shein, zikiwemo barabara, hospitali, elimu na maji pamoja na kusambazwa umeme karibu kila kona.

Katika ziara yake hiyo Kinana amewataka viongozi wa dini na Serikali kukemea kitendo cha CUF kuwaita wanaohamia CCM makafiri.


Naye Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alimpongeza Komredi Kinana kwa ziara yake, kwamba imekuwa ya mafanikio makubwa na imewapa somo na moyo wa kuimarisha chama visiwani.

 Komredi Kinana akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo, ambapo aliwataka wananchi kuwahoji wabunge wa CUF na Wawakilishi kuhusu matumizi ya fedha za jimbo sh. milioni 40 wanazipatiwa kwa ajili ya maendeleo ya jimbo.
 Mkazi wa Mjimbini, akitafakari hotuba ya Komredi Kinana.
 Komredi Kinana akiwa na baadhi ya viongozi wengine wa chama na serikali wakiomba dua walipozuru kaburi la aliyekuwa Makamu wa Rais, Hayati Dk. Omari Ali Juma eneo la Wawi Digilini, Wilaya ya Chakechake, Pemba.

 Komredi Kinana akikagua shamba la matikiti maji katika shamba la wajasiriamali katika Kijiji cha Wambaa kwa Anzani. Pia alishiriki kupanda mbogamboga katika shamba hilo.
 Mkungu wa ndizi ukiwa katika shamba la vijana  katika Kata ya Chokochom ambapo Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana alishiriki kupanda migomba.


 Balozi wa CCM Shina namba 1, Ame Vuai Shein, akifungua kikao alipotembelewa na Komredi Kinana eneo la Kadarani Chokocho , Jimbo la Mkanyageni, Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba.Ame ni mdogo wa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.

 Vijana wa CCM wakiimba wimbo wa kuwakumbuka viongozi waliotangulia mbele ya haki, wakati Kinana alipofika kuzindua kambi yao eneo la Chokocho, Jimbo la Mkanyageni, Pemba.


 Baadhi ya wananchi wakisikiliza kwa makini wakati Komredi Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU