LIGI DARAJA LA KWANZA: POLISI WAJERUHI MASHABIKI, YUPO ALIYEKATWA SIKIO, ALIYECHANWA TAKO NI UKATILI WA KUTISHA

MASHABIKI wa  Majimaji  ya Songea juzi  walijikuta katika wakati mgumu pale waliposhambuliwa na askari  Polisi wa kikosi  cha kutuliza ghasia na  baadhi yao wakilazwa hospitali ya mkoa wa Ruvuma(HOMSO) wodi ya majeruhi wakitibiwa baada ya  majeraha  ya kipigo kutoka kwa askari.
Askari hao ambao  walionekana  kutumia nguvu zaidi kuliko mashabiki ambao waliokuwepo  kiwanjani hapo, baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi Daraja la kwanza (FDL) kati ya Majimaji  na Kurugenzi  ya Mufindi, mchezo  ambao ulimalizika  kwa timu hizo kufungana bao 1-1, mchezo huo  ulifanyika kwenye uwanja wa  Majimaji  mjini hapa.
Katika mchezo huo  Majimaji  ndio walikuwa wakwanza  kujipatia bao la kuongoza katika dakika ya 12 na Ditram Nchimbi kwa mpira wa kichwa, kabla ya Kurugenzi kusawazisha bao hilo  katika 54 Asili Mkondya aliyeingia kuchukua nafasi ya Stanley Msangila, na Majimaji walikuwa wakicheza mbele ya Mkufunzi wao wa kiufundi na Mkurugenzi wa kituo cha michezo cha Symbion  cha jijini Dar es Salaam, Stuward Hall.
Pamoja  na mashabiki  wa Majimaji  kulalamika  kuwa mashabiki wa Kurugenzi  wamekuwa na tabia ya kuzishambulia timu pinzani zinapocheza kwenye uwanja wao wa nyumbani  kwa kushirikiana na askari polisi wa wilaya hiyo, kitu ambacho askari wa kikosi hicho wakahisi huenda mashabiki hao wakalipiza kisasi wanachokifanya mashabiki wenzao  wa timu pinzani.
Polisi walianza kurusha mabomu baada ya mashabiki wa Majimaji  kumzomea  Mbunge wao, Emmanuel  Nchimbi  wakati  akitoka uwanjani kushuhudia  mchezo huo, baada ya Mbunge huyo kuwapungia mkono mashabiki hao  akiwataka  watulie,huku mashabiki wao walijibu  hatukutaki  tuachie tuwafunze adabu hao  Kurugenzi , kauli ambayo ilionekana iliwaudhi  Polisi  na kuanza kutumia  nguvu  kupiga mabomo na kutembeza  kipigo  pasipo sababu ya kimsingi kama kwa binadamu mwenye akili mwenye utashi wa kutambua baya na zuri.

wachezaji wa kurugenzi wakitolewa uwanjani kwa gari la polisi
Pamoja na Polisi kuwaondosha uwanjani  wachezaji wa Kurugenzi na viongozi wao salama bado waliendelea kutengeneza chuki kwa wananchi  kwa kuendelea kuwashambulia, kwani askari hao walihama ndani ya uwanja wa Majimaji na kuhamia mitaani  kupiga  wananchi wasiokuwa na makosa kama  soko la Manzese ambapo waliingia na kuanza kuwashambulia wafanyabiashara  pamoja na wanunuzi  ambao waliingia katika soko hilo kutafuta mahitaji yao.

Baadhi ya mashuhuda wetu ambao walikuwa wakifuatilia  unyama wa askari  hao alidai hasira za askari hao   zilimalizika maeneo ya Bombambili umbali wa kilometa mbili kutoka ulipo uwanja wa Majimaji ambapo  walipiga mabomo na kuwashambulia wananchi wasiokuwa na hatia na kurejea kambini kwao, huku  wakiwaacha wananchi wa Songea katika mshangao mkubwa juu ya hatima ya chombo chao  kilichopewa dhamana ya kulinda usalama wa maisha ya raia na mali zao.

Mmoja wa wahanga hao pamoja na mwandishi wa mtandao wa www.jamvila habari.com alijikuta katika wakati mgumu pale alipolazimishwa  kulala chini kifudifudi huku askari mmoja  akimlinda kwa kumwekea bunduki ya aina ya SMG kisogoni wakimzuhia asipige picha za tukio hilo jinsi linavyoendelea pamoja na kumpa vitisho wangeweza kuondosha uhai wake mara moja, alidai alitii amri hiyo kwa lengo la kuokoa uhai wa maisha yake.

Mwandishi wa gazeti  pia aliweza kupata bahati na kuzungumza  na baadhi ya majeruhi  ambao wamelazwa katika hospitali ya mkoa(HOMSO) wakipatiwa matibabu akiwemo mtangazaji wa kituo cha Radio cha mjini hapo (Jogoo Fm) ambaye amelazwa wodi namba mbili kitanda namba tatu, Hossam  Ulaya alidai alishambuliwa na askari  saba wa kikosi hicho wakati  akijaribu kuwasalimisha  wachezaji  wa timu ya mkoa ya wanawake, baada ya Polisi kuwatembezea kichapo  kisichokuwa na sababu, huku mmoja ya kati ya hao wachezaji amelazwa wodi namba  tano ambaye amejitambulisha kwa jina la Arasha Chande

Mtangazi huyo alisema kichapo hicho kilimkuta baada ya kuona wachezaji hao wa timu ya mkoa ya wanawake  wakichalazwa bakora na askari ambao wakiongozwa na mkuu wa kituo cha Polisi cha wilaya ya Songea,  ambaye alimtaja kwa jina moja la Mashimbi ambaye alikwenda kwa ajili ya kuwasalimisha wachezaji hao, wakati  huo  anakwenda kuwasalimisha akiwa amefuatana na mjumbe wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la mpira wa miguu nchini(TFF), James Mhagama.
 Alisema pamoja na kichapo hicho bado aliweza kumshuhudia mjamzito  wakimshambulia kwa  marungu katika  maeneo mbalimbali ya mwili wake huku akilia  kwa maumivu  na kumtaja askari mmoja wa kike ambaye na alikuwa akishiriki unyama huo alidai aliweza kunukuru jina moja   la Jojina, na baadaye askari huo alikwenda na kuanza kumfariji kwa kumpa pole wakati wamemuumiza.

 Alisema askari hao pamoja na vitendo vya vya kinyama kubwa zaidi alidai waliweza kumvamia mtoto wa jinsia ya kiume ambaye alidai anaweza kuwa na umri wa miaka saba kwa kumshambulia kwa marungu, mateke na kupelekea kumsababishia maumivu , alidai licha ya mtoto huo kuangua kilio askari hao waliendelea kumpa kichapo  aliokolewa na kikundi cha vijana ambao walijitoa muhanga  kwa kuwavamia askari hao kwa kuwarushia mawe na kuamua kumuacha na kukimbia huku mtoto huyo akiwa tayari amepoteza fahamu

Hata hivyo  habari za kitelejensia  ambazo  zimenaswa na gazeti hili huenda vita hiyo ikaendelea Januari 24 mwaka huu, wakati Mlale JKT watakapokutana na Kurugenzi ya Mufindi katika mchezo wa ligi hiyo ya FDL ambao utakuwa wa kulipiza kisasi kati ya wananchi na jeshi la Polisi ambapo wananchi wanajipanga kwa mashambulizi, gazeti hili litaendelea kuwapatia nini kinachojili juu ya tukio hilo ambalo linahisiwa huenda likapelekea kutokea kwa mauaji.

Na baadhi ya wadau wa  soka wa Songea walizungumza na gazeti hili wengi wao wamelitupia lawama  jeshi la Polisi wamekuwa wakitumia nguvu nyingi kulikoni akili na maharifa, huku wakidai hata nchi ikiingia kwenye machafuko yatakuwa yanasababisha na askari wa jeshi la Polisi na si jeshi la wananchi, kwani michezo ujenga umoja mshikamano wa kindugu  na pia inaendeleza kudumisha  amani na utulivu wetu  tulionao Watanzania kwa sasa huku wakidai Serikali wanatakiwa walione hilo.

Hata hivyo Katibu mkuu wa chama cha soka mkoa wa Ruvuma (FARU) Ahamed Challe amesikitishwa na maamuzi ya jeshi la Polisi la kutumia nguvu kuliko akili, alidai ilikuwa haina sababu ya kuwashambulia wananchi na kuwajeruhi  wakati  wachezaji wa kurugenzi walikuwa wamewaondoa uwanja wakiwa chini ya ulinzi wao kwa amani na utulivu, baada ya hapo nao wangeondoka na wangeendelea na majukumu yao mengine ya kiusalama badala ya kuingia mitaani na kuanza kuwashambulia wananchi bila ya sababu.

 Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikheli hakuweza kupatikana kuelezea tukio  hilo lakini ameweza kunukuliwa wakati akiingia hospitali ya mkoa, kumtakia  hali huyo mtangazaji wa  kituo cha Jogoo Fm, Hossam Ulaya kuwa taarifa alizozipata kutoka kwa maofisa wake walidai wananchi walikuwa na lengo la kuwafungia milango askari wake ndani ya uwanja wa Majimaji kwa lengo la kuwashambulia, kitu ambacho si kweli  huo ni uongo mtupu wanania ya kujitetea mbele ya Kamanda wao.

    

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*