MBEYA CITY YAITANDIKA BAO 2 – 1 SIMBA KATIKA LIGI KUU YA TANZANIA BARA

Wachezaji wa Mbeya City wakiwa wamembeba kocha wao 'Juma Mwambusi' baada ya kupata ushindi wa bao 2 - 1 dhidi ya wekundu wa Msimbazi Simba
Wachezaji wa Mbeya City wakiwa wamembeba kocha wao ‘Juma Mwambusi’ baada ya kupata ushindi wa bao 2 – 1 dhidi ya wekundu wa Msimbazi Simba
Katika mechi ya ligi kuu Tanzania bara iliyopigwa katika uwanja wa Taifa leo, wekundu wa Msimbazi Simba wamejikuta wakivutwa sharubu baada ya kuchezea kichapo cha bao 2 – 1 dhidi ya Mbeya City ya jijini Mbeya.
Timu ya Simba ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza kupitia mchezaji wake, Ibrahim Ajib, hata hivyo Simba walionekana kupwaya hivyo kutoa nafasi kwa Mbeya City kuongeza mashambulizi hivyo kupata bao la kusawazisha mnamo dakika ya 77 kutoka kwa mchezaji wao Kibopole.
Mbeya City ilipata bao la pili na la ushindi kwa njia ya mkwaju wa penalti baada ya mlinda mlango wa Simba, Peter Manyika kumuangusha mchezaji wa Mbeya City na mchezo kumalizika kwa Mbeya City kushinda 2 – 1 dhidi ya Simba.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.