MBUNIFU WA MAVAZI WA KIMATAIFA, SHERIA NGOWI AMVALISHA RAIS MPYA WA ZAMBIA

 
 
 
Rais mpya wa
Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum  (Presidential suit)
iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini Tanzania
Sheria Ngowi
akikagua gwaride rasmi kabla ya kuapishwa katika sherehe
za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini
Lusaka-Zambia. Guy Scott, of Scottish 
 

Rais mpya wa
Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential
suit)iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini
Tanzania Sheria
Ngowi
akila kiapo cha kuwa Rais Mpya wa Zambia  katika
sherehe
za zilizofanyika  jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini
Lusaka-Zambia. Guy Scott, of Scottish
 Rais mpya wa
Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential
suit)iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini
Tanzania Sheria
Ngowi
akitia saini Hati Maalum Muda mfupi baada ya
kuapishwa katika sherehe
za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini
Lusaka-Zambia.
 
 Rais mpya wa
Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential suit)
iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini Tanzania
Sheria Ngowi
akipokea salaam Maalum Kutoka kwa Rais wa Mpito wa Zambia Guy Scotts
Muda mfupi baada ya   kuapishwa katika sherehe
za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini
Lusaka-Zambia.
 
  Rais mpya
wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential
suit)iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini
Tanzania Sheria Ngowi  akiwa na Mkewe Eshter Lungu  Muda
mfupi baada ya   kuapishwa katika sherehe
za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini
Lusaka-Zambia.
—–
 
Na Mwandishi
Wetu

Mbunifu wa mavazi
wa kimataifa, Sheria Ngowi ameendelea
kuipeperusha bendera ya Tanzania kupitia kipaji chake cha ubunifu wa
mavazi baada ya kumvalisha Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu katika sherehe
za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini
Lusaka-Zambia.

Rais Lungu 58,
aling’arisha sherehe hizo baada
ya kuvaa suti rasmi (Presidential suit) rangi ya bluu, shati jeupe na
tai nyekundu zilizobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa kimataifa, Sheria
Ngowi. Lungu aliambatana na mke wake, Eshter Lungu walipokuwa wanaingia
viwanjani hapo huku wakisindikizwa na ulinzi mkali.
 
Akizungumza baada
ya hafla hiyo, Sheria Ngowi alisema
amefurahi kupata nafasi ya kipekee ya kumvalisha Rais Lungu katika sherehe
za kuapishwa kwake na kusema ni hatua kubwa katika kazi yake kama mbunifu
wa mavazi wa kimataifa.

“Hii ni hatua
kubwa katika kazi yangu ya ubunifu
wa mavazi, namshukuru Mungu kwa kipaji alichonipa kinachoweza kunitambulisha
na kunifanya niaminike hata kufikia hatua ya kuvuka mipaka ya Tanzania
na kumvalisha Rais mpya wa Zambia, Mheshimiwa Edgar Lungu”, alisema
Ngowi.
 
Mbunifu Ngowi
alisisitiza kuwa juhudi, nidhamu, bidii
na kumweka Mungu mbele ndio chachu ya mafanikio katika kila utendaji
wa kazi zake akiwa na malengo ya kuipeleka kazi yake katika nyanja za
kimataifa hata kutambulika katika sekta ya ubunifu wa mavazi duniani
kote.
 
Hafla hiyo
ilihudhuriwa na aliyekuwa Rais wa muda
wa Zambia, Guy Scott na mke wake Charlotte, Mwenyekiti wa jumuiya ya
maendeleo ya nchi za kusini(SADC), Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, baadhi
ya viongozi wa juu wa Zambaia na nchi mbalimbali pamoja na wananchi
wake.
 
Mbunifu huyo
ameendelea kuonyesha na kudhihirisha
kuwa Tanzania ni nchi yenye vipaji vinavyoweza kuiletea nchi ya Tanzania
sifa na kuinua uchumi wake katika sekta mbalimbali. Hii si mara ya kwanza
kwa mbunifu huyo kukata mawingu kuitangaza nchi yetu, kwani ni miongoni
mwa wabunifu mashuhuri kutoka Afrika wanaopata fursa kuonyesha ubunifu
wa mavazi yao katika maonyesho ya kimataifa kama vile New York Fashion
Week nchini Marekani na Mercedes Benz fashion Week nchini Afrika
Kusini.

Hii ni changamoto
pia kwa wabunifu wa Tanzania kuziwania
fursa zilizopo na pia kuongeza juhudi ili kutangaza na kupeleka kazi
zao katika soko la kimataifa kama vile Sheria Ngowi alivyofungua
mlango.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA