MRISHO MPOTO : FURAHA ILIYOJEE BAADHI YA MATAIFA KUTUMIA MUZIKI WANGU KAMA SEHEMU YA MASOMO KATIKA VYUO VYAO

Muziki wa Mrisho Mpoto ‘Mjomba’ umezidi kupasua anga la kimataifa na kubisha hodi katika mataifa mbalimbali kwa kutumika kama sehemu ya masomo katika sekta za elimu ikiwemo vyuoni.
Mrisho Mpoto
Wanafunzi wa chuo cha Wales Marekani wakitazama video ya Mpoto ikiwa ni moja ya somo
Msanii huyo ambaye ni balozi wa lugha ya kiswahili,  ameshea moja ya video kwenye ukurasa wake wa Instagram ikiwaonyesha wanafunzi wa chuo cha Wales kilichopo nchini Marekani wakijifunza somo la kuzuia na kupambana na ujangilia kupitia video ya wimbo wake ”Deni la Hisani” ambayo amemshirikisha  Peter msechu kwenye kiitikio.
Faraja iliyoje baadhi ya mataifa duniani kazi zangu ni sehemu ya masomo katika vyuo vyao, asante watanzania kwa kuendelea kunijenga kimataifa, #Njoouichukue j3”, aliandika Mpoto kwenye mtandao wa Instagram

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.