P-SQUARE WAKUBALI UWEZO WA DIAMOND

      

MWACHENI Diamond aitwe Diamond! Hiyo kauli pekee unayoweza kuisema kufuatia wakali wa muziki wa R&B kutoka Nigeria, Peter na Paul Okoye ‘P-Square’ kuukubali uwezo wa kimuziki wa bwa’mdogo kutoka Tandale, Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Ijuma Wikienda linakupa mchapo hatua kwa hatua (HABARI KWA HISANI YA .http://www.globalpublishers.info/)
Bwa’mdogo kutoka Tandale, Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa madansa wake ndani ya Lagos, Nigeria.
NI LAGOS, NIGERIA
Wakali hao walionesha kumpigia saluti Diamond baada ya kukutana naye kwenye tamasha la utoaji wa Tuzo za Wanamichezo Bora Afrika lililofanyika Lagos, Nigeria, usiku wa kuamkia Januari 9, mwaka huu.
WALIANZIA HOTELINI
Kwa mujibu wa chanzo kilichoambatana na Diamond nchini humo, saa chache kabla ya shoo kuanza, P-Square walimuibukia kwenye Hoteli ya Eko aliyofikia jijini humo na kummwagia pongezi nyingi sambamba na kumshauri baadhi ya vitu vya kimaendeleo.
‘Diamond Platnumz’ akifurahia jambo na Peter Okoye wa ‘P Square’.
TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo hicho kilisema, P-Square walionekana kuvutiwa zaidi na juhudi binafsi za Diamond kiasi cha kuweza kuipeperusha bendera ya Afrika Mashariki katika levo za kimataifa.
“Jamaa walipomuona tu hotelini waliguswa sana na juhudi zake binafsi maana wanatambua jinsi gani muziki ulivyokuwa mgumu kuuvusha nje ya nchi yako lakini kwa kuwa Diamond ameweza, walimpigia saluti,” kilisema chanzo hicho.
ARUHUSIWA KOLABO
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data za ndani kwa kusema, mbali na kumpigia saluti, P-Square walionesha wako tayari kumsapoti Diamond kwa kumpa nafasi ya kufanya nao kazi yaani kolabo.
“Wamempa nafasi ya kufanya naye kazi pale atakapojisikia kutokana na mipango yake, kama akiamua kufanya sasa au baadaye ni uamuzi wake lakini jamaa (P-Square) hawana kinyongo naye lengo lao ni kuona muziki wa Afrika unateka dunia,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
‘Diamond Platnumz’ akiwa na Paul Okoye wa ‘P Square’.
“Walimwambia the way (namna) alivyo na juhudi kwenye kazi yake anatambulika Nigeria utafikiri ni msanii kutoka Nigeria, walimpa mbinu zao za namna walivyopigana hadi kufika hapo walipo.”

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI