Kijana Andrew Mlaki kutoka kikundi cha Akili ni Mwanga akielezea vijana wenzake (hawapo pichani) shughuli zinazofanywa na kikundi chake baada ya kikundi hicho kutembelewa na wawezeshaji waliofika Wilaya ya Mwanga kuhamasisha vijana na kuwapa elimu kuhusu ujuzi na stadi za maisha. Kushoto ni mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Ester Riwa.
wa Wilaya ya Mwanga Bibi Subira Mfanga akizungumza na vijana walioshiriki semina ya uhamasishaji kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana Mkoani Kilimanjaro katika Wilaya ya Mwanga.
Wawezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Maafisa Ushirika na Maafisa Vijana kutoka Wilaya ya Mwanga na Moshi Vijijini, katika picha ya pamoja na baadhi ya Vijana wa Wilaya hizo walioudhuria semina ya uhamasishaji kwa vijana kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana katika Wilaya ya Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Bw. Jamhuri David Willium (katikati) akisikiliza mrejesho kutoka kwa wawezeshaji wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo waliofika ofisini kwake baada ya kufunga semina ya uhamasishaji kwa Vijana wa Wilaya za Mwanga na Moshi Vijijini hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Bw. Jamhuri David Willium kushoto akipokea Sera ya Maendeleo ya Vijana kutoka kwa mwezeshaji wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa baada ya kufunga semina ya uhamasishaji kwa Vijana wa Wilaya za Mwanga na Moshi Vijijini hivi karibuni.
(Picha zote na : Genofeva Matemu – Maelezo)
Comments