TANZANIA YASHIRIKI KATIKA MKUTANO WA KUMI WA MAENDELEO YA TAKWIMU AFRIKA NCHINI UGANDA.

      

unnamedWashiriki kutoka Tanzania wakisikiliza kwa makini mambo yanayoendelea katika Mkutano wa Kumi wa Maendeleo ya Takwimu Afrika uliofanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Speke Munyoyo Kampala, Uganda. Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Prof. Innocent Ngalinda, katikati ni Meneja wa Takwimu za Kilimo Titus Mwisomba kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu Prof. Milline Mbonile. unnamed1Washiriki wengine kutoka Tanzania wakisikiliza kwa makini mambo yanayoendelea katika Mkutano wa Kumi wa Maendeleo ya Takwimu Afrika uliofanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Speke Munyoyo Kampala, Uganda.  Kushoto ni Meneja wa Sensa ya Watu na Makazi Irenius Ruyobya akifuatiwa na Dkt. Camilius Kasalla kutoka Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika.
unnamed3Waziri Mkuu wa Uganda Mhe. Ruhakana Rugunda akimpongeza Mwandishi wa Kitabu cha Mapinduzi ya Takwimu Afrika Prof. Ben Kiregyera baada ya kukizindua leo kwenye Mkutano wa Kumi wa Maendeleo ya Takwimu Afrika uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Speke Munyoyo Kampala, Uganda unnamed4. Waziri Mkuu wa Uganda Mhe. Ruhakana Rugunda akiwahutubia washiriki mbalimbali kutoka barani Afrika (hawapo pichani) wakati wa Mkutano wa Kumi wa Maendeleo ya Takwimu Afrika uliofanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Speke Munyoyo Kampala, Uganda. (PICHA NA VERONICA KAZIMOTO – KAMPALA)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA