TIMU YA WATAALAMU KUTOKA WIZARA YA UCHUKUZI WATEMBELEA OFISI ZA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA(TCAA)

      

unnamedMeneja wa Kitengo cha taarifa za Usalama wa Usafiri wa Anga, Bw. Deodore Mushi akitoa maelezo ya namna ya mashine mbalimbali zinazotumika katika chumba maalum cha kutolea taarifa za usafiri wa Anga zinavyofanya kazi, kwa wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi, waliotembelea katika ofisi hizo leo asubuhi kufanya tathimini ya utoaji wa huduma katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA). Wa Kwanza kulia ni Afisa Usafirishaji kutoka Wizara ya Uchukuzi, Bw. Biseko Chiganga (aliyevaa koti jeusi), wa pili kushoto kwa Chiganga ni Afisa Usafirishaji, Bw Benjamin Mbimbi na tatu kutoka kushoto ni Afisa Usafirishaji, Bw. Said Marusu.
unnamed1Meneja wa Kitengo cha Uongozaji Ndege, Mwanajuma Kombo, akifafanua jambo kwa wataalamu kutoka Wizara ya Uchukuzi, waliotembelea kituo cha kuongozea ndege leo asubuhi kufanya tathmini ya utoaji wa huduma katika usafiri wa Anga katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA).
unnamed3Meneja wa Kitengo cha Uongozaji Ndege, Mwanajuma Kombo akiwaonyesha wataalamu kutoka Wizara ya Uchukuzi, karatasi inayoonyesha aina ya ndege, mahali inapokwenda na muda itakaotumia inakokwenda, katika kituo cha uongozaji ndege kilichoko Katika uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere leo asubuhi wakati wataalam hao walipotembelea kituo hicho. unnamed5Meneja wa Kitengo cha Uongozaji Ndege, Mwanajuma Kombo (mwenye kilemba chekundu), akiwaelezaa wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi, namna waongoza ndege wanavyotumia rada na kuelekeza marubani sehemu za kupita, wakati wataalam hao walipotembelea kituo hicho leo asubuhi kufanya tathmini ya utoaji wa huduma katika usafiri wa anga katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere.
(Picha na Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi).

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

𝙂𝘼𝙈𝙊𝙉𝘿𝙄 𝙆𝘼𝘾𝙃𝙀𝙕𝘼 𝙆𝙄𝘽𝙄𝙉𝙂𝙒𝘼.