Kufuatia mkutano wa Watanzania waishio ujerumani na Rais wa Tanzania Mhe
Jakaya Kikwete, Mweyekiti wa umoja wa watanzania
Ujerumani UTU e.V Bw,
Mfundo Peter Mfundo ameeleza matarajio ya Watanzania waishio Ujerumani,
alifafanua kwamba japokuwa Rais Kikwete amebakisha muda mfupi katika
uongozi wake lakini Umoja huo unaamini kuwa madam Rais Kikwete ameona
umuhimu wa kufanya mkutano na Watanzania wanaoishi ujerumani basi
anaweza akatekeleza mahitaji ya Watanzania hao.
Bw Mfundo alifafanua
pia hoja za msingi ambazo zitaibuka kwenye mkutano huo ni pamoja na
Utekelezwaji wa upatikianaji wa fursa zilizopo Tanzania kwa watanzania
wanaoishi Ujermani,(Diaspora) aidha aliendelea kueleza kwamba hoja
nyingine ya msingi ni kutaka kujua msimamo wa serikali juu ya Uraia
Pacha, kwani Watanzania wanaoishi ujerumani wana kiu kubwa ya kujua
swala la Uraia pacha limefikia wapi.
Akiendelea kuongea na Mtangazaji
Grace Kabogo kupitia sauti ya Radio Deutsche Welle idhaa ya kiswahili
Bw. Mfundo alisema kutokana na Vijana wengi wa Tanzania kujiajiri
kupitia Muziki na kuupiga vita umasikini, Umoja wa Watanzania Ujerumani
Utamuomba rais Kikwete kusaidia kupitisha msamaha wa kodi kwa Vyombo
vya Muziki ili kuwawezesha Vijana wa Tanzania kumudu ununuzi wa vifaa
hivyo, Bw. Mfundo alieleza moja ya changamoto wanazozipata ni pale
umoja huo unapokosa mawasiliano ya moja kwa moja na Idara ya Diaspora
Tanzania.
Comments