WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO AFANYA ZIARA KATIKA MKOA WA SIMIYU KUKAGUA MIRADI YA UMEME NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI

      

Waziri wa Nishati na Madini  Profesa Sospeter Muhongo  anafanya ziara katika mikoa ya Shinyanga, Tabora na Simiyu lengo likiwa ni kukagua miradi ya umeme  vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati  Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Shirika la  Umeme Nchini (Tanesco)unnamed1dWaziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akipokelewa na baadhi ya watendaji kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Kanda ya Ziwa na Nishati na Madini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza. Profesa Muhongo anafanya ziara katika mikoa ya Simiyu, Tabora na Shinyanga lengo likiwa ni kukagua miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Taneesco.
unnamed2dWaziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega kabla ya kuanza ziara katika wilaya hiyo ili kujionea utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini pamoja na kuzungumza na wananchi.
unnamed3dMkazi wa kijiji cha Ihale kilichopo wilayani Busega mkoani Simiyu  ambaye jina lake halikupatikana mara moja akiuliza maswali mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na wananchi (hawapo pichani) mara Waziri alipofanya mazungumzo na wananchi wa kijiji hicho ili kusikiliza kero zao.
unnamed4dWaziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo kwenye mkutano na wananchi wa kata ya Ijitu iliyopo wilayani Busega
unnamed5dWaziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akitoa maelekezo kwa Meneja wa Tanesco- Kanda ya Ziwa Mhandisi Joyce Ngahyoma ( wa mwisho kushoto) ya kuitaka Tanesco kuongeza kasi ya usambazaji wa umeme vijijini.
unnamed6dWaziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo   katika mkutano wake na wananchi wa kijiji cha Bushigwamala wilayani Busega (hawapo pichani)Sehemu ya umati wa wananchi wa kata ya Kalemala wilayani Busega waliojitokeza kwenye mkutano na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo wakifuatilia kwa makini hotuba yake.
unnamed7d unnamed8dMeneja wa Tanesco- Kanda ya Ziwa Mhandisi Joyce Ngahyoma, akifafanua jambo mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na wananchi wa kijiji cha Nyamikoma wilayani Busega (hawapo pichani)
unnamed9dDiwani wa Kata ya Ijitu iliyopo wilayani Busega Vumi Magoti akielezea kero za umeme katika kata yake mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa pili kutoka kushoto), viongozi na wananchi (hawapo pichani)
mzu
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akitoa maelekezo kwa mtaalamu kutoka kampuni ya Symbion iliyopewa kazi ya kujenga miundombinu ya umeme katika kijiji cha Nyamikoma kilichopo wilayani Busega Bw. Steve Thomson (kushoto)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

𝙂𝘼𝙈𝙊𝙉𝘿𝙄 𝙆𝘼𝘾𝙃𝙀𝙕𝘼 𝙆𝙄𝘽𝙄𝙉𝙂𝙒𝘼.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI