Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na MNEC wa CCM Taifa,Bwa.Daudi Ismaili pamoja na baadhi
ya wanachama wa CCM,mara baada ya kuwasili katika mkutano wa Wajumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM,Wilayani Chake Chake,Mkoa wa Kusini Pembaa
mapema leo.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu
ya CCM,Wilayani Chake Chake,Mkoa wa Kusini Pemba mapema leo,ambapo pia
Ndugu Kinana alipokea taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.
Pichani
Kulia ni Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba,Mh.Mwanajuma Maggid Abdallah
akizungumza jambo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana (pichani
shoto),wakati Ndugu Kinana alipokwenda kushiriki ujenzi wa Taifa wa tawi
la CCM Mchangani katika jimbo la Wawi,wilaya ya Chake Chake-Mkoa wa
Kusini Pemba.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pichani shoto akishiriki ujenzi wa tawi la CCM
Mchangani katika jimbo la Wawi,wilaya ya Chake Chake-Mkoa wa Kusini
Pemba akiwa sambamba na Wananchi na wanachama wa CCM.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza mbele ya Wananchi wa
Uwandani katika jimbo la Wawi,kabla ya kukagua utekelezaji wa Ilani
chama cha Mapinduzi na kushiriki Ujenzi wa Madarasa ya Skuli ya Uwandani
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana sambamba na Wananchi wakishiriki ujenzi wa
Madarasa ya Skuli ya Uwandani,katika jimbo la Wawi,wilaya ya Chake
Chake,Mkoa Kusini Pemba.Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa mbele ya katibu
Mkuu Ndugu Kinana,imeeleza kuwa mradi wa ujenzi wa jengo hilo
litakalokuwa na jumla ya vyumba sita,litagharimu kiasi cha shilingi
milioni 18 zitakazomilisha mradi huo.
Katibu
Mkuu wa CCM na ujumbe wake pamoja na wananchi wakikatiza kwenye shamba
la miti linalosimamiwa na Kikundi cha Utunzaji Mazingira kiitwacho
Hatugombani Cooperative,kilichopo Kilindi,Wilaya ya Chake Chake,mkoa wa
Kusini Pemba.Kikundi hicho kina jumla ya Wanachama wapatao 49,ambapo
shughuli kubwa ya kikudi hicho ni utunzaji wa mazingira kwa upandaji
miti ya Mivinje,Mikaratusi,Mikungu na Mitondoo.Mradi huo wa kuhifadhi
Mazingira una eneo la eka 20,ambapo mpaka sasa mradi huo una thamani ya
shilingi Milioni 40 na zaidi
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akishiriki kupanda mti katika shamba la miti linalosimamiwa na Kikundi cha Utunzaji Mazingira
kiitwacho Hatugombani Cooperative,kilichopo Kilindi,Wilaya ya Chake
Chake,mkoa wa Kusini Pemba.Kikundi hicho kina jumla ya Wanachama wapatao
49,ambapo shughuli kubwa ya kikudi hicho ni utunzaji wa mazingira kwa
upandaji miti ya Mivinje,Mikaratusi,Mikungu na Mitondoo.Mradi huo wa
kuhifadhi Mazingira una eneo la eka 20,ambapo mpaka sasa mradi huo una
thamani ya shilingi Milioni 40 na zaidi
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akielekea katika kijiji cha
Chanjamjawiri,jimbo la Chake Chake akiwa ameongoza na viongozi
mbalimbali wa CCM Wilaya na Mkoa CCM Kusini Pemba kushiriki upandaji wa
miche ya Mikarafu,katika ushirika wa uitwao Hatukosani wenye jumla ya
Watu 25.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kuotesha miche ya Mikarafuu katika
bustani ya kikunndi cha Hatukosani,wakati alipotembelea na kukagua
shughuli zinazofanywa na kikundi hicho chenye wanachama wapatao 25
kilichopo Chanjamjawiri-Chake Chake mkoa wa Kusini Pemba.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipewa taarifa ya kikundi cha Ushirika cha
Jitihada Mbele cha Ufugaji wa Samaki chenye jumla ya wanachama
10.Kikundi hicho kilianzishwa kwa lengo la Ufugaji wa samaki ili waweze
kujikwamua kiuchumi na pia kusimamia sera ya chama cha CCM,ikiwemo
kujikusanya kwa pamoja ili kuanzisha vikundi vya ushirika kwa ajili ya
kujiajiri wenyewe.Kwa Mujibu wa Msomaji wa taarifa alieleza kuwa mradi
huo wa samaki una jumla ya thamani ya shilingi milioni 10.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishirik kuchimba moja ya mabwawa ya
wanakikundi hao wa Jitihada Mbele akiwa sambamba na baadhi ya wananchi
na wanachama wa CCM.
Mbunge
wa Viti Maalum Pemba,Mh.Faida Bakari akifafanua mambo mbalimbali
yaliyomo ndani ya Katiba mpya inayopendekezwa,inayotarajiwa kupigiwa
kura mnamo Aprili 30,Mbunge huyo ameawata Wananchi wa Pemba kuipigia
kura ya ndio katiba hiyo ili ipite,kwani ina mambo mengi mazuri kwa
Zanzibar
Baadhi ya Wanachi wakifuatilia kwa makini mkutano wa hadhara uliofanyika mapema jioni ya leo Pujini Kunvini Chake Chake mkoa wa Kusini Pemba.
Mbunge wa Viti Maalum,Mh.Asha Abdul Haji akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika mapema jioni ya leo Pujini Kunvini Chake Chake mkoa wa Kusini Pemba,ambapo pia Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana aliwahutubia wananchi wa eneo hilo.
Baadhi
ya Wanachama wa CCM wakishangilia jambo katika mkutanno wa hadhara
uliofanyika kwenye uwanja wa Pujin Kumvini-Chake Chake mkoa wa Kusini
Pemba.
Mfuasi wa Chama cha CUF Ghalib Bedui Khamis akikabidhi kadi yake kwa katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na kukabidhiwa kadi mpya ya uanachama wa CCM.
Mfuasi
wa Chama cha CUF Said Abdallah Ibrahim akionesha kadi yake ya zamani
kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kabla ya kukabidhi na kupewa kadi
mpya ya uanachama wa CCM,mbele ya Wananchi katika mkutano wa hadhara
uliofanyika Pujini Kunvini Chake Chake mkoa wa Kusini Pemba.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia Wananchi katika
mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye uwanja wa Pujini Chake
Chake,mkoa wa Kusini Unguja
Comments