BREAKING NEWS-ZITTO KABWE ASHINDWA KESI DHIDI YA CHADEMA


Hatimaye chama cha CHADENA kimeshinda kesi dhidi ya aliyekuwa mwanachama wake Zitto Kabwe.Mahakama Kuu (Mziray,Judge) amekubaliana na hoja za wanasheria wa CHADEMA  za pingamizi dhidi ya case hiyo kwamba ilifunguliwa bila kufuata utaratibu wa kisheria. Mahakama Kuu imeipa CHADEMA gharama zote za kuendesha case hiyo. Kwa maana hiyo hakuna shauri lolote Mahakamani kwa sasa kuhusu suala hilo.


Aidha, Mahakama imeamuru Zitto alipe gharama zote za kesi.
Wanasheria wa chama, Peter Kibatala na John Mallya na Tundu Lisu wanatarajiwa kuongea  na Vyombo vya Habari hii leo.


 Mwaka jana Zitto Kabwe aliweka pingamizi mahakamni kuzuia kikao cha Kamati Kuu kumjadili.
Hoja yake ni kupinga kuitisha kamati kuu kabla shauri lake kusikilizwa na Baraza Kuu.
Alidai anataka mahakama iagize kamati kuu ya CHADEMA kutojadili suala lake mpaka baraza kuu likae kuamua rufaa yake.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.