CHAMA CHA WENYE ULEMAVU WA NGOZI (ALBNO) MKOA WA MBEYA WAKANUSHA SIASA KUHUSIKA NA MATUKIO YAO.


Katibu wa Chama cha Walemavu wa ngozi(Albino) Mkoa wa Mbeya, William Simwali akizungumza na vyombo vya habari

Katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya (kulia) akiwa sambamba na wakuu wa mikoa ya Mbeya na Rukwa kumjulia hali Mtoto Baraka Cosmas (hayupo pichani)aliyekatwa aliyekatwa kiganja cha mkono wake na watu wasiojulikana na kutokomea nacho.


Waandishi wa habari wakiwa wodini alikolazwa Mtoto Baraka Cosmas katika Hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya kufuatia kukatwa kiganja chake cha Mkono wa kulia na watu wasiojulikana kisha kutokomea nacho.

CHAMA cha Walemavu wa Ngozi (Albino)Mkoa wa Mbeya kimesema matukio yanayoendelea ya kukata viungo vyao pamoja na mauaji hayahusiani kabisa na masuala ya uchaguzi bali ni imani za kishirikina zilizowatawala wananchi.

Hayo yalibainishwa hivi karibuni na Katibu wa Chama hicho Mkoa wa Mbeya William Simwali kufuatia kukatwa kiganja cha mkono wa kulia mtoto Baraka Cosmas(6) na watu wasiojulikana na kasha kutokomea nacho kusikojulikana kijijini kwao Chipeta wilayani Sumbawanga Mkoa wa Rukwa hivi karibuni  na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya.

Simwali alisema watu wengi hivi sasa wanalinganisha matukio hayo na masuala ya uchaguzi jambo ambalo sio la kweli kutokana na kushamili katika vipindi ambavyo hakuna uchaguzi bali yanatokana na wakati ambapo Serikali na Taasisi mbali mbali kutoa matamko ya kupinga mauaji ya Albino.

Alisema mara ya kwanza matukio ya mauaji ya albino yalishamiri katika Kanda ya Ziwa mwaka 2008 kipindi ambacho hakina uchaguzi wowote pamoja na Miaka mingine iliyofuata ambapo aliitaka Serikali kufanya utafiti wa kina kubaini wahusika na kuwachukulia hatua kali kama inavyofanya kwa majangili.

Alisema matukio hayo Serikali inapaswa kulaumiwa kutokana na kutokuchukulia kwa umakini katika kuyakomesha kama ilivyo kwa matukio mengine ambapo Serikali ikitoa muda mambo hayo hutekelezwa ndani ya muda huo tofauti na ukomeshaji wa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

Alisema Rais alitoa aagizo la kuwaondoa majangili wanaoua tembo jambo ambalo lilifanikiwa lakini pia agizo lake la ujenzi wa maabara katika shule za sekondari nchi nzima lilivyofanikiwa ndani ya muda mfupi hivyo kushangaza kushindwa kulitafutia ufumbuzi suala la mauaji ya Albino.

Naye mweka hazina wa Chama hicho Mkoa wa Mbeya, Claud Mwakyoma alisema ili suala hilo likomeshwe ni bora watu wenye ulemavu wakawekewa ulinzi maalumu ikiwa ni pamoja na kutengewa eneo lao ili waangaliwe kwa ukaribu.

Alisema kama suala la ulinzi litashindikana afadhali Albino wote wakakusanywa nchi nzima na kupelekwa gerezani ili wakaishi kwa uhuru zaidi kutokana na kuwepo kwa ulinzi kwa masaa 24 jambo ambalo litasaidia kukomesha vitendo hivyo kabisa.

Mwisho.

Na Mbeya yetu.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.