IMETOSHA Campaign : Mwanahabari Ajitolea Kupambana na Wauaji wa Albino



Balozi wa kujitolea wa kampeni ya
mapambano dhidi ya mauaji ya albino, Henry Mdimu (wa pili kulia)
akizungumza na vyombo vya jhabari. Kampeni hiyo inajulikana kwa jina la
Imetosha. Balozi wa kujitolea wa kampeni ya mapambano dhidi ya mauaji ya albino, Henry Mdimu (wa pili kulia) akizungumza na vyombo vya jhabari. Kampeni hiyo inajulikana kwa jina la Imetosha.Mchoraji maarufu na mmoja wa
wanakamati wa kampeni za imetosha Masoud Kipanya (kulia) akizungumza na
DW. Mchoraji maarufu na mmoja wa wanakamati wa kampeni za imetosha Masoud Kipanya (kulia) akizungumza na DWMwenyekiti wa Tanzania Bloggers
Network (TBN), Joachim Mushi (kulia)  akihojiwa na DW mara baada ya mkutano
wao. TBN imeunga mkono kampeni hizo zinazoongozwa na balozi wa kujitolea wa
mapambano hayo, Henry Mdimu. Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Joachim Mushi (kushoto) akihojiwa na DW mara baada ya mkutano wao. TBN imeunga mkono kampeni hizo zinazoongozwa na balozi wa kujitolea wa mapambano hayo, Henry Mdimu.Baadhi ya wajumbe wa kampeni za
imetosha wakipata picha za ukumbusho mara baada ya kuzungumza na
wanahabari. Baadhi ya wajumbe wa kampeni za imetosha wakipata picha za ukumbusho mara baada ya kuzungumza na wanahabariMkutano na wanahabari ukiendelea.  
Mkutano na wanahabari ukiendelea
 Na Mwandishi Wetu MMOJA wa watu wenye ulemavu wa ngozi, albino na mwanahabari shupavu kutoka kampuni ya Mwananchi Communication, Henry Mdimu amejitolea kuwa balozi wa hiyari kupinga mauaji ya kikatili ya watu wenye albino yanaoendelea nchini. Bw. Mdimu ambaye ameungwa mkono na baadhi ya marafiki na watu wanaokerwa na vitendo hivyo, ikiwemo Chama cha Bloggers nchini, Tanzania Bloggers Network (TBN) amesema ameamua kufanya hivyo baada ya kushuhudia ndugu zake wakiteseka kwa muda mrefu dhidi ya mauaji hayo. 
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Balozi Mdimu amesema lengo lake kuu ni kuhakikisha anazunguka pamoja na marafiki watakao muunga mkono na kutoa elimu kwa kuanzia Kanda ya Ziwa ili tatizo hilo lisiendelee kuenea nchi nzima. Akifafanua zaidi alisema mauaji ya watu wenye albino yanaichafua Tanzania hivyo atahakikisha anaisaidia Serikali kupambana na watu wenye imani hizo za kipuuzi ili kuondoa doa linaloichafua nchi yetu ambayo imekuwa na sifa ya amani dunia nzima. "...Nimeamua kufanya hivi baada ya kushuhudia ndugu zangu wakiteseka kwa muda mrefu. 
Awali nilishindwa kuanzisha harakati hizi nikiamini kuna vyombo vinavyohusika na utetezi wa watu wenye ulemavu wa ngozi." "...Hivyo nimeamua niweke jitihada zangu binafsi niisaidie Serikali yangu katika kuondoa doa hili linaloichafua Nchi yetu yenye sifa ya Amani duninia nzima. Hivyo nawaomba Watanzania wenzangu mniunge mkono tukishirikiana na Serikali ili mauaji haya yakome," alisema Mdimu. "Kutokana na ushawishi nilionao kama Mwandishi, Mtangazaji wa redio na Blogger naamini nitaleta mabadiliko makubwa katika kuhakikisha haki ya kusihi kwa ndugu zangu inaheshimiwa na kubaki historia. Salamu zangu ziwafikie wanyanyasaji, wauaji na wenye kufanya dhihaka kwa watu wenye ulemavu wa ngozi kuwa IMETOSHA." Akifafanua zaidi alisema kwa uchunguzi wake wa awali umebaini ukosefu wa elimu juu ya watu wenye ulemavu wa ngozi ndio chanzo cha tatizo hilo kukua na hatimaye kuuana kwa imani za kishirikina. "...Hivyo basi, silaha ya Elimu ni sehemu kubwa ya haraki hizi," alisisitiza Balozi huyo wa kujitolea. 
Aidha alisema kuendesha harakati hizo alizozipa jina la 'IMETOSHA' elimu itatolewa kwa njia ya sanaa, na washauri nasaha pamoja na kundi la wanamuziki ambao pia wataandaa nyimbo mbalimbali za kutoa mafunzo ya kutokomeza ukatili huu. Alisema wasanii ambao hadi sasa wamejitokeza kuunga mkono kampeni hizo ni paoma na Jhikoman, Kassim Mganga, Profesa J, Ray C, Fid Q, Roma Mkatoliki na Dami Msimamo. Hata hivyo alisema bado pia anaamini nguvu ya vyombo vya habari ikiungana na kampeni hizo wanaweza kufanikiwa zaidi hivyo kuomba ushirikiano katika kuhakikisha vinapaza sauti kutokomeza mauaji hayo ya kikatili. **Imeandaliwa na www.thehabari.com *

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI