Kanali Mstaafu. Issa Selemani afungua kikao cha Kazi kwa Viongozi,Watalaam wa Elimu Mkoani Katavi


      

1
Mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanali Mstaafu. Issa Selemani Njiku akifungua kikao cha Kazi kwa Viongozi,Watalaam wa Elimu Mkoani Katavi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo  Dkt. Ibrahim Msengi hayupo pichani kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa shule ya sekondari Inyonga Wilayani Mlele kushoto kwa Mkuu wa Wilaya ni Afisa Elimu Mkoa Ernest Hinju aliyeshikakidevu akitafakari jambo.
2
Wajumbe wa Kikao kazi cha sekta ya elimu Mkoani Katavi wakifuatilia mjadala wa mada zilizokuwa zikiwasilishwa na Afisa Elimu Mkoa Mkoa Mkoa wa Katavi namna ya uboreshaji wa elimu na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.
…………………………………………………
Na Kibada Ernest Kibada-Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Ibrahimu Msengi ameagiza wanafunzi wote waliohitimu Elimu ya Msingi mwaka 2014 na kufaulu kwa kuchaguliwa kujiunga ba Elimu ya Sekondari waripoti katika  shule walizopangiwa  wahudhurie  hadi wamalize elimu ya sekondari.
Alitoa kauli hiyo katika hotuba yake iliyosomwa na kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanali Mstaafu Issa Seleman NJiku  wakati akifungua kikao kazi cha Viongozi,Wataalamu wa Elimu Mkoani Katavi  kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano Shule ya Sekondari iliyonga wilayani Mlele.
Mkuu huyo wa Mkoa amehimiza kukomeshwa kwa  watoro   mashuleni  wanafunzi walioacha shule wasakwe na kurudishwa shuleni ili waendelee na masomo,akasema watoro hao ni wale ambao wenzao wanaendelea shule kwa sasa.
Amewaagiza Viongozi hao kuhakikisha uandikishaji wa wanafunzi Elimu ya Awali unafanyika na kila Shule ya Msingi kuwe na Darasa la kwanza Elimu ya Awali, miaka inavyosonga mbele uandikishaji unashuka sana  na hasa kwa elimu ya Awali.
Akizungumzia ukamilishaji wa ujenzi wa maabara kila Shule ya Sekondari iwe na  maabara inayofanya kazi na ifikapo machi 30 mwaka huu Halmashauri  zinatakiwa zimkabidhi  Maabara hizo zikiwa  zimekamilika kila kitu ,kuanzia majengo,vifaa na miiundombinu yote muhimu inayohitajika na iwe inafanya kazi.
Awali  Afisa Elimu Mkoa wa Katavi Ernest Hinju katika taarifa yake ya   Mkoa kuhusu maendeleo ya taaluma alisema kuwa Mkoa  umepiga hatua kubwa kimaendeleo kwenye  sekta ya Elimu kitaaluma, katika matokeo ya kuhitimu elimu ya Msingi,matokeo ya darasa la saba mwaka 2014 Mkoa umefanya vizuri.
Hinju alieleza kuwa matokeo yanaonesha Halmashauri ya Mji wa Mpanda ilishika nafasi ya kwanza kitaifa kwa kuwa na ufaulu wa asilimia 90, hivyo kuufanya  Mkoa ulishika nafasi ya  11 kitaifa  ulipanda kwa nafasi tatu 3 kitaifa.
 Takwimu zinaonesha kuwa matokeo kwa ku darasa nne kwa mwaka 2014 ambapo Mkoa umefaulisha wanafunzi 8514 kati yao wanafunzi 9931 sawa na asilimia 85.73 hali ambayo ni mafanikio makubwa.
Kwa upande wa  matokeo ya darasa saba 2013 Mkoa ulifaulisha wanafunzi 3769 kati ya 8142 sawa na asilimia 46 ya na hivyo kushika nafasi ya 13 kati ya Mikoa 25.kwa Mwaka 2014 matokeo ya darasa la saba mkoa umefaulisha wanafunzi 4419 kati ya 7240 sawa na asilimia 61.04 na hivyo mkoa kushika nafasi ya 11kati ya mikoa 25,Mkoa umeshika nafasi ya 3 kitaifa na  Halmashauri ya MJi wa Mpanda
 Akizungumzia mtihani wa kidato nne mkoa umepata ufaulu wa asilimia 69 na kufikia  malengo na  shule ya sekondari usevya ilishika nafasi  38 kati ya shule 268  za kitaifa katika matokeo ya mtihani  kidato cha sita.
Pamoja na mafanikio hayo pia zipo zipo changamoto kadha ambazo zinaikabili sekta ya Elimu Mkoa baadhi ya changamoto hizo  ni uhaba wa madawati,upungufu wa madarasa na nyumba za walimu, maabara, baadhi ya shule kutoa chakula mashuleni hali inayochangia kushusha taaluma mashuleni
 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

𝙂𝘼𝙈𝙊𝙉𝘿𝙄 𝙆𝘼𝘾𝙃𝙀𝙕𝘼 𝙆𝙄𝘽𝙄𝙉𝙂𝙒𝘼.