KINANA AAHIDI KUUNUSURU MLIMA UNAOCHIMBWA MAWE YA KUBADILISHANA NA MAJI ARUMERU MASHARIKI

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akilakiwa na akina mama waliobeba ndoo tupu ikiwa ni ishara ya kuelezea tatizo la maji linalowakabili wakazi wa Kijiji cha Shimbundu  Jimbo la Arumeru Mashariki,wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Wakazi wa eneo hilo wamedai kuwa wamekuwa na tatizo hilo la maji tangu wazaliwe kiasi cha kuwafanya walazimike kubadilishana maji na kokoto zinazotokana na kuuvunja mlima wa mawe uliopo kijijini hapo.

Komredi Kinana ambaye katika ziara yake ameambatana na Katibu wa Itikadiu na Uenezi, Nape Nnauye, amewaahidi wananchi wa eneo hilo kuwasaidia kukamilisha mradi wa maji utakaogharamiwa na Serikali ili mlima huo unusurike. Eneo hilo kwa hivi sasa linaoongozwa na Mbunge Joshua Nassari wa Chadema.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Akina mama wakiusimamisha msafara wa Komredi Kinana iliwaeleza tatizo la kutopatikana maji tangu wazaliwe katika Kijiji cha Shimbungu, Jimbo la Arumeru Mashariki, mkoani Arusha.
 Akina mama wakiwa na ndoo wakati wa mkutano na Komredi Kinana karibu na mlima unaopasuliwa mawe kupata kokoto za kubadilishana maji.
 Wazee wa kabila la Wameru, wakimvisha mgolole ikiwa ni ishara ya kumkaribisha kuwa mzee wa kimila wa kabbila hilo.
 Nape akivishwa mgolole kiwa ni heshima ya wazee kumkaribisha kimila katika Kijiji cha Shimbungu
 Bibi kizee adelela Muungule (78)  akiwa miongoni mwa akina mama wa Kijiji cha Shimbungu, Jombo la Arumeru Mashariki. Bi Adelela amesema kuwa tangu utotoni wamekuwa wakiteseka kupata maji ambvapo walikuwa wanatembea umbali mrefu kuata maji katika mto mmoja uliopo mbali na kijiji hicho.
 Komredi Kinana akisalimiana na wauguzi wa Hosptali ya Wilaya ya Tengeru, alipokwenda kukagua jengo jipya la upasuaji pamoja na ujenzi wa jengo la kuhifadhia maiti..
 Komredi Kinana akitoka kukagua jengo la upasuaji katika hospitali hiyo.

 Komredi Kinana akiruka msingi alipokwenda kukagua jengo la kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Tengeru, Jimbo la Arumeru Mashariki, Mkoa wa Arusha.
 Baadhi ya walimu wa Chuo cha Ualimu cha  Patandi wakiwa na bango linaloelezea kuwa aliwahi kusoma hapo, ambapo awali ilikuwa inaitwa West Meru Middle School. Kinana alisoma katika shule kuanzia darasa la tano hadi la saba kati ya mwaka 1967-1968.
 Komredi Kinana akielezea mazingira ya eneo la shule hiyo aliyosoma jinsi ililivyokuwa tofauti na lilivyo sasa.
 Komredi Kinana akitia saini kwenye kitabu cha wageni cha chuo hicho.
 Msafara wa Kinana ukipita karibu na majengo ya chuo hicho enzi hizo kilivyokuwa shule ya kati alisoma Komredi Kinana.
 Wananchi wakimlaki Komredi Kinana alipowasili katika Kijiji cha Sing'isi kuzungumza na wananchi

 Komredi Kinana akizungumza na wananchi ambapo aliwahidi kuumaliza mgogoro wa ardhi kati ya wana Kijiji na Wawekezaji wanaohodhi ardhi na kuwaacha wananchi wakiteseka kwa kutokuwa na mashamba.

 Komredi Kinana akishiriki ujenzi wa jengo la mashine ya kukobolea mbunga katika  Kata ya Usa River Lekitatu, Jimbo la Arumeru Mashariki


 Komredi Kinana akizungumza na mmoja wa vijana wa Kata ya Mbuguni ambapo yeye alizaliwa, alipofika kukagua mradi wa maji na kuzungumza na wananchi
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara ambapo alikemea kitendo cha Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nayalandu kutembea na viongozi wa dini  kwenye misafara yake mikoani, ili wawe wanamsafisha na tuhuma za kushindwa kutatua migogoro ya ardhi kati ya Hifadhi za Taifa na Wananchi.


 Komredi Kinana akimpongeza aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Wilaya ya Arumeru, John Palangyo kwa kitendo chake cha kuihama CUF na kujiunga na CCM, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Mbuguni, Wilayani Arumeru.
 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano huo
 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano uliofanyika Kata ya Mbungu, alikozaliwa yeye.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagana na Mkuu wa Kwanza wa Majeshi mstaafu wa kwanza, Jenerali Sarakikya katika Kijiji cha , Nkoanekoi, Jimbo la Arumeru Mashariki baada ya kumaliza kuhutubia na kutatia kero mbalimbali za wananchi wa kijiji hicho kinachokabiliwa na tatizo la maji, barabara mbovu pamoja na umeme.
 Komredi Kinana akivishwa mgogole na wazee wa Kata ya Mbuguni

Wazee wa Kata ya Mbuguni wakimvisha zawadi ya mgolole, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ikiwa ni heshima ya wazee hao wa Kata aliyozwa Komredi Kinana.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI