Msafara wa Kinana ukivuka mto ulipokuwa unaingia katika Kata ya Mkoka wakati za ziara yake katika Jimbo la Kongwa.
Katibu Mkuu wa CCM akitembea pekupeku alipovua viatu wakati akienda kushiriki kupapalia shamba la Alizeti la la Kijiji cha Iduo Wilayani Kongwa.
Komredi Kinana akiwa na viongozi wengine wa CCM pamoja na wananchi wakishiriki kupalilia shamaba la alizeti la Kijiji cha Iduo, wakati wa ziara yake katika Jimbo la Kongwa, mkoani Dodoma.
Komredi Kinana akilakiwa na kikundicha ngoma wakati wa mapokezi ya kuingia Jimbo la Kongwa, akitokea Wilaya ya Mpwapwa, wakati wa ziara yake mkoani Dodoma. |
Komredi Kinana akisaidia kumtwisha ndoo ya maji Subilaga Bukuku baada ya kuzindua mradi wa Maji katika Kijiji cha Malali, wilayani Kongwa leo.
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kongwa, Job Ndugai 9kulia0 akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana walipotoka kushiriki ujenzi wa vyumba vya madarasa na hosteli ya Shule ya Msingi wilayani Kongwa.
Kikundi cha ngoma cha akina mama kikitumbuiza wakati Komredi Kinana alipokwenda kushiriki ujenzi wa zahanati ya Kijiji Njoge, jimboni Kongwa.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika Kijiji cha Njoge ambapo alishiriki ujenzi wa Zahanati ya Kijiji hicho.
Komredi Kinana akishiriki ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Njoge, Jimbo la Kongwa. Zahanati hiyo imejengwa kwa nguvu za wananchi.
Komredi Kinana (kulia) akijadiliana jambo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye (katikati) pamoja na Mkuu wa Kitengo cha CCM Mawasiliano ya Umma, Daniel Chongolo.
Komredi Kinana akiwapungia wananchi alipokuwa akiingia kuhutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Mkoaka, Jimbo La Kongwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Luteni Chiku Galawa akisalimia wananchi wakati wa mkutano wa hadhara katika Kata ya Mkoka.
Kikundi cha ngoma za utamaduni cha Kifaru kikitumbuiza wakati wa mkutano, huo.
Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa akihutubia katika mkutano huo
Mama mwenye jamii ya kimasai akimkabodhi zawadi ya fimbo Komredi Kinana
Wananchi wakimsikiliza kwa makini wakati Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Mkoka
Komredi Kinana akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Chadema Wilaya ya Kongwa, na Katibu Mwenezi wa chama hicho wa Kata ya Ngomai,Mwakang'ata Nyanje akitangaza kujiunga na CCM katika mkutano huo. Kushoto ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.
Nape Nauye akiwataka wananchi wanaokiunga mkono Chama Cha Mapinduzi kunyoon mikono juu wakati wa mkutano huo. CCM katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Jimbo la Kongwa imeshinda kwa asilimia 99.
Comments