KINANA AMMWAGIA SIFA LUKUKI MBUNGE WA MTERA, LUSINDE 'KIBAJAJI' KWA UCHAPAKAZI HODARI

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Mbunge wa Jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde wakiwa na furaha baada ya kuvishwa migolole na wazee wa kabila la Wagogo ikiwa ni ishara ya kuwaheshimu, baada ya mkutano wa hadhara kumalizika katika Kijiji cha Manzase, Kata ya Fufu, Jimbo la Mtera, wialayni Chamwino, Mkoa wa Dodoma.

Katika mkutano huo, Komredi Kinana alisema kuwa licha Mbunge anayejulikana kwa jina la utani la Kibajaji na sasa Mtalimbo  kuwa msemaji hodari mwenye kujenga hoja ndani na nje ya  Bunge pia ni mchapakazi hodari anayeliletea maendeleo jimbo lake. 

Komredi Kinana yupo mkoani Dodoma kwa ziara ya kuimarisha uhai wa chama , kugagua miradi ya maendeleo ya inayotekelezwa kwa kufuata Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, na kusikiliza kero za Wananchi pamoja na kuzitafutia ufumbuzi. PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Komredi Kinana akishirikiana na Mbunge Lusinde kufyatua tofali katika Shule ya Msingi Lowassa,katika Kijiji cha Muungano, Jimbo la Mtera, Dodoma
 Kinana akiendesha harambee ya kuchangia mabati, simenti kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa Shule ya Msingi Lowassa, katika Kijiji cha Muungano, Jimbo la Mtera.
 Mbunge wa Jimbo la Mtera, Livingston Lusinde akimwangalia Komredi Kinana akipampu maji ya kisima kujaza kwenye ndoo wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji katika Kiji cha Mvumi Mission jimboni humo.
 Komredi Kinana akisaidia kumtwisha ndoo ya maji mmoja wa akina mama wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji uliojengwa kwa msaada wa Taasisi ya Oxfarm katika Kijiji cha Mvumi Mission, Jimbo la Mtera.
 Mbunge wa Jimbo la Mtera, Lusinde akimtwisha ndoo ya amaji mmoja wa akina mama baada ya uzinduzi wa mradi huo.
 Wajumbe wa Mkuutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Jimbo la Mtera, wakiwa na furaha wakati wa kumlaki Komredi Kinana katika mkutano huo uliofanyika Kijiji cha Mvumi Mission.
 Mmoja wa wajumbe wa mkutano huo,Nyambile Myetumbi akizungumzia uzembe wa wahudumu na madaktari wa Hospitali ya Mvumi Mission, pamoja na mauaji yanayoendelea katika Jimbo hilo la Mtera.
 Komredi Kinana akilakiwa kwa ngoma alipowasili katika Shule ya Msingi ya Suli jimboni Mtera ambapo alishiriki kupiga lipu katika shule hiyo inayojengwa kwa msaada wa Taasisi ya Goog Neibour katika Kijiji cha Suli, Kata ya Fufu.
 Mbunge wa Jimbo la Mtera, Lusinde akielezea jinsi alivyopigania kupata msaada wa ujenzi wa shule hiyo ya Suli, kutoka Taasisi ya Good Neibour ya Korea Kusini ambapo alisema mambo yote hayo yanafanyika kutokana na kuwepo sera nzuri za CCM.

 Komredi Kinana akiondoka baada ya kushiriki kupiga lipu katika moja ya vyumba vya madarsa ya shule hiyo.

 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Luteni Chiku Galawa, akishiriki kupanda mti katika Hosteli ya Shule ya Sekondari ya Fufu iliyojengwa kwa msaada wa Taasisi ya Good Neibour ya Korea Kusini, jimboni Mtera.
 Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Farida Mgomi akishiriki kupanda mti katika Hosteli hiyo
 Komredi Kinana akiwa amekaa kwenye kitanda baada ya kukagua Hosteli ya Shule ya Sekondari Fufu katika Jimbo la Mtera
 Kinana akiondoka baada ya kukagua mradi wa maji ambao hadi sasa haujakamilika kutokana na Serikali kutompatia mkandarasi  fedha za kumalizia mradi huo katika Kijiji cha Manzase jimboni humo. Kinana ameahidi kulifuatilia jambo hilo kwa wahusika ili fedha zitolewe kwa ajili ya kukamilisha mradi huo muhimu unaotegemewa na zaidi ya watu 8000.
 Mbunge wa Jimbo la Mtera, Lusinde akisisitiza kwamba Serikali iwakumbuke wananchi wa Kata ya Fufu kukamilisha haraka mradi  huo wa maji
 Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara na kuwataka wananchi kuachana kabisa na vyama vya upinzani kwani havina sra nzuri za kuwasaidia, bali chama pekee chemnye uwezo wa kuwasaidia katika masuala ya maendeleo ni CCM.
 Mwenhyekiti wa Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa akihutubia kabla ya kumkaribisha Komredi Kinana kuzungumza na hadhara hiyo.
 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano huo ambapo aliahidi kuwa chamgamoto mbalimbali zinalolikumba jimbo hilo atasaidia kuzitafutia ufubuzi ambazo ni ukosefu wa maji, minara ya simu na umeme.
 Mmoja wa wanachama wapya wa CCM akipatiwa kadi ya chama hicho wakati wa mkutano huo.
Mbunge wa Jimbo la Mtera, Lusinde akivishwa kwa heshima mgolole wakati wa mkutano huo.
 Komredi Kinana akishiriki kupanda mti katika Hosteli ya Shule ya Sekondari Fufu, Jimbo la Mtera, wilayani Chamwino
Mbunge wa Jimbo la Mtera, Lusinde akishiriki kupanda mti katika hosteli hiyo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA