KINANA;WEZI, MAFISADI HAWAFAI KUONGOZA NCHI


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiendesha toroli lenye zege aliposhiriki kwenye ujenzi wa daraja la Kisongo, Jimbo la Arumeru Magharibi, Arusha wakati wa ziara ya siku tisa iliyomalizika leo mkoani Dodoma ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Komredi Kinana ambaye katika ziara hiyo ameambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akihutubia leo katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Olturumet, Arumeru Magharibi,  amesema kuwa viongozi wezi na mafisadi hawafai kuongoza nchi na kuongeza kuwa mwizi ni mwiztu tu, hata awe wa CCM ama Chadema wote hawafai.PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Komredi Kinana akimwaga zege kwenye daraja aliposhiriki ujenzi wa daraja hilo la Kisongo.
 Wananchi wa Kijiji cha Nduruma, Jimbo la Arumeru, wakiwa na mabango ya kulalamikia kitendo cha viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru, kukwepesha bomba la maji badala ya kwenda kwa wananchi limelekezwa kwenye mashamba kwa ajili ya umwagiliaji.

Katika sakata hilo, Katibu Mkuu;, Kinana alitumia busara kutuliza ghasia kwa kuwaamuru vingozi wa wilaya hiyo kuhakikisha kilio cha wananchi kinapatiwa ufumbuizi kwa kuwapelekea maji. Alisema kuwa baada ya mwezi mmoja atatembelea ghafla mradi huo wa maji

 Mmoja wa wanakijiji wa Kijiji cha Nduruma, akitoa maelezo ya jinsi mkandarasi na viongozi wa halmashauri wanavyodaiwa kuugeuza mradi huo kwa matumizi ya kumwagilia mashamba badala ya  kuwapeklekea wananchi maji
 Wananchi wakioonesha kwa mbali eneo ambalo maji yanatakiwa kuwepo katika Kijiji cha Nduruma.
 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano huo
 Vijana wa CCM, wakitumbuiza wakati Komredi Kinana alipowasili Kata ya Mlangarini kushiriki ujenzi wa Kituo cha Afya cha Manyire, Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha.

 Komredi Kinana akishiriki ujenzi wa jengo la Kituo cha Afya cha Mlangarini, Wilaya ya Arumeru, Arusha.
Komredi Kinana akipiga lipu moja ya majengo ya shule ya Sokon 11, wilayani Arumeru, Arusha\
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Ole Medeye akielezea mbele ya wananchi kuhusu utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ulivyofanyika katika jimbo hilo.
 Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Arusha, Onesmo Nangole akihutubia katika mkutano huo, ambapo aliwapongeza Komredi Kinana na Nape kwa ujasiri wao wa kutembea nchi nzima kukiimarisha chama na kuwataka watumuishi wa serikali,mawaziri pamoja na waziri mkuu kuiga mfano  wao kwa kutoka kwa maofisini kwenda vijijini kuwatumikia wananchi. 
Komredi Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.