KOMREDI KINANA AANZA ZIARA MKOANI KILIMANJARO

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara huku mvua ikinyesha kwenye Uwanja wa CCM, Sanya Juu wilayani Siha,wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Komredi Kinana ambaye katika ziara ya siku tisa mkoani Kilimanjaro, ameambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, ameusifu uongozi wa wilaya mpya ya Siha kwa kupiga hatua za kimaendeleo hasa katika kuwaletea maji safi na salama, uboreshaji wa huduma za afya na miundombinu.

 Chipukizi wa CCM, akimvisha skafu, Komredi Kinana wakati wa mapokezi kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Nuru, alipowasili kutoka mkoani Arusha.
 Chipukizi wakiimba wakati wa mapokezi hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas  Gama akisalimiana na Komredi Kinana
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama akihutubia wakati wa mapokezi ya msafara wa Komredi Kinana katika Shule ya Sekondari Nuru, wilayani Hisa, Kilimanjaro.
Mbunge wa Jimbo la Siha,Aggrey Mwanry akielezea miradi mbalimbali iliyotekelezwa katika jimbo hilo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho
Komredi Kinana akishiriki kutandaza zege katika jengo la bwalo la chakula katika Shule ya Sekondari ya Nuru.
Kmoredi Kinana akikagua daraja Embukoi wakati wa ziara hiyo
Msafara wa Komredi Kinana wilayani Siha
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiangalia bwawa la umwagiliaji la Kishisha Kata ya Evaen
Komrediu Kinana akiwa na Mbunge wa Jimbo la Hisa Aggrey Mwanry alipokwenda kukagua bwawa la umwagiliaji la Kishisha
Komredi Kinana akikagua bwawa la umwagiliaji la Kishjsha
Komredi Kinana akionesha eneo la kufungulia maji katika bwawa hilo la Kishisha.

Komredi Kinana akisalimiana na waguzi wa Hospitali mpya ya Wilaya ya Siha
Kinana akiwa na Mwanry (kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Idd Juma akikagua hospitali hiyo.
Komredi Kinana akikagua maabara ya hospitali hiyo
Mbunge wa Jimbo la Siha, ambaye pia ni Naibu Waziri wa TAMISEMI, Aggrey Mwanry akielezea miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa katika jimbo hilo
Kinana akihutubia wananchi mjini Sanya Juu huku mvua ikinyesha
Wananchi wakisikiliza hotuba ya Komredi Kinana huku wakiwa wamejikinga na mvua
Gama, Mwanry na Juma wakisikiliza hotuba ya Komredi Kinana huku mvua ikiwanyeshea
Gama akimkumbatia Komredi Kinana abaada ya kufurahishwa na hotuba
Komredi Kinana akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Idd Juma kwa kuwa mmoja wa watu waliosaidia ujenzi wa jengo la CCM Wilaya ya Siha.
Jengo jipya la CCM wilaya ya Siha.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.