KOMREDI KINANA AHUTUBIA USIKU KATIKA ZIARA YAKE WILAYANI CHEMBA, KONDOA


 Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara kwa kuwaliza wananchi ni wanangapi wanaiunga mkono CCM katika Uwanja wa Shule wa Itolwa, Wilaya ya Chembe, Kondoa, Mkoa wa Dodoma, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua Ilani ya Utekelezaji ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015. Pia katika ziara hiyo inayofanyika katika mikoa mitatu ya Dodoma, Arusha na Kilimanjaro, Kinana atasikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara, katika Kata ya bItolwa, wilaya mpya ya Chemba, Dodoma wakati wa ziara hiyo ya siku 27 katika mikoa hiyo mitatu
 Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dodoma, Alhaji Adam Kimbisa akiungana na wananchi kucheza ngoma ya asili ya kabila la Warangi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Itolwa, Wilaya mpya ya Chemba.
 Komredi Kinana akipigilia msumari kwenye kenchi la Jengo la Ofisi ya Serikali ya Kijiji cha Babayu wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Chemba, Dodoma.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Luteni Chiku Galawa na Mbunge wa Jimbo hilo, Juma Nkamia.
 Komredi Kinana akiendelea na kati za kutengeneza Kenchi. Nyuma yake ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Luteni Chiku Galawa na Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dodoma, Alhaji Adam Kimbisa wakishiriki kupiga lipu wakati wa ukarabati wa Josho la mifugo katika Kata ya  Gwandi, wilayani Chemba, Dodoma. Josho hilo liliwahi zinduliwa na aliyekuwa Rais wa Tbanzania, Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere mwaka 1969.Kata hiyoina zaidi ya mifugo 14,000.
 Komredi Kinana akikagua ukarabati wa josho hilo

 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Chemba katika Makao makuu ya wilaya hiyo..

 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akivishwa mkufu wa asili wa kabila la Warangi wakati wa mapokezi katika Kijiji cha Paranga ambapo walishiriki ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto pamoja na kupanda miti
 Komredi Kinana akifanyiowa mambo ya kimila ya kabila la Warangi alipowasili katika Kijiji cha Paranga kushiriki nujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto pamoja na kupanda miti.
 Komredi Kinana akiwa amefanyiwa mambo ya kimila katika Kijiji cha Paranga.
 Komrdi Kinana akifanyiwa tena mambo ya kimila katika Kijiji cha Songolo ambapo alipatiwa taarifa ya mradi wa maji ambao kwa kipindi kirefu ujenzi wake umekuwa ukisuasua. Kinana ameahidi kulifanyia msukumo tatizo hilo katika ngazi za juu za Serikali.
 Diwani wa Kata  ya Goima, Mwanaharusi Bato (kushoto) akiungana na wananchi kucheza ngoma ya asili ya kabila la Warangi wakati Komredi Kinana alipowasili katika Kijiji cha Songolo, wilayani Chemba
 Akina  mama wakimwimbia wimbo Komredi Kinana alipowasili katika Kijiji cha Songolo wilayani Chemba
 Komrdi Kinana akizungumza na Wananchi katika Kijiji cha Songolo
 Komredi Kinana akilakiwa kwa nderemo katika Kijiji cha Mapngo wilayani Chemba
 Komredi Kinana akishangiliwa katika Kijiji cha Mapango
 Komredi Kinana akihutubia katika miutano uliofanyika katika Kata ya Itolwa, wilayani Chemba.
 Sehemu ya umati wa watu katika mkutano huo
 Komredi Kinana akimkabidhi hundi ya sh, mil 10 kiongozi wa kikundi cha vijana wajasiriamali cha Tumaini Silic, zilzotolewa na Serikali kwa ajili ya kuendeleza mradi wa ufugaji nnyuki. Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imetoa zaidi ya sh. mil. 50 kwa vikundi vya vijana wilayani humo
 Komredi Kinana akihutubia usiku kwa msaada wa taa za magari alipofika kukagua ujenzi wa Soko la Kimataifa lka Mazao katika Kata ya Mrijo, wilayani Chemba.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.