KOMREDI KINANA AIVURUGA CHADEMA ROMBO

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akilakiwa na madiwani wa chama hicho alipowasili wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro.shiriki kucheza ngoma ya kabla la Wapare alipowasili katika Kijiji cha Mwaniko, Ugweno, wilayani Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
 Wananchi wakishangilia walipomuona Komredi Kinana ayewasili kuanza ziara ya siku moja wilayani Rombo.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia wakati wa mapokezi na kuwataka wananchi kujisasahihisha kwa kosa walilolifanya la kuchagua Mbunge wa Chadema ambaye kwa miaka mitano hakjawafanyia maendeleo yoyote, hivyo mwaka huu wamchague Mbunge na Rvais wa kupitia CCM WENYE UWEZO WA KULIENDELEZA JIMBO HILO.
 Komredi Kinana akihutubia mkutano wakati wa mapokezi eneo la Mkuu Rombo.
 Baadhi ya Waendesha Bodaboda  900 wakiwa na vyeti vayo vya Bimba ya Afya baada ya kukabidhiwa na Komredi Kinana wakati wa mapokezi.
 Mmoja wa viongozi wa vikundi 20 vya wajasilriamali akikabidhiwa mkataba pamoja na hundi ya fedha  ambapo vikundi vyote hivyo vilikabidhiwa jumla ya sh. mil. 47.
 Viongozi wa vikundi vya wajasiriamali wakiwa na mikataba yao baada ya kukabidhiwa na Komredi Kinana.
 Komredi Kinana akizindua jengo jipya la Ofisi ya CCM Wilaya ya Rombo
 Komredi Kinana akizungumza jambo na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha juisi na maji cha Bella alipotembelea kiwanda hicho wilayani Rombo
 Komredi Kinana akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kiwanda cha juisi cha Belle wilayani Rombo.
 Komredi Kinana akiweka shada la maua kwenye kaburi walimozikwa wanafunzi 38 waliokufa baada ya hosteli yao kuteketea kwa moto katika Shule ya Sekondari ya Shauritanga, wilayani Rombo mwaka 1994
 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya Rombo wakisikiliza kwa makini wakati Komredi Kinana akihutubia.
 Komredi Kinana (kushoto) akishirki kuvuta waya wakati wa ujenzi wa mradi wa Umeme  wa Kirongo Samanga wilayani Rombo

 Wafanyakazi wa Tanesco wakifunga waya kwenye nguzo wakati wa ujenzi wa mradi wa umeme wa Kirongo Samanga wilayani Rombo
 Komredi Kinana akikagua ujenzi wa mradi wa Maji katika Kata ya Kahe uliogharimu zaidi ya sh. mil. 500 zilizotolewa na Serikali Kuu kuondoa tatizo la maji wilayani Rombo. Mradi huo ambao umekamilika kwa asilimia 90 utakuwa na uwezo wa kuhudumia zaidi ya wakazi 7000 ambao awali walikuwa wanategemea maji kutoka Kenya. Jimbo hilo linaongozwa na Mbunge wa Chadema.
 Komredi Kinana akiunganisha bomba la maji wakati wa uzinduzi wa mradi huo
 Komredi Kinana akimsaidia kumtwisha ndoo ya maji mmoja wa akina mama wa Kata Kahe baada ya kuzindua mradi huo.
 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Tarakea, Rombo na kuitaka Serikali kupunguza masharti ya wananchi wa mipakani kufanya biashara zao katika mipaka nchi zinazopakana.
 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano huo wa hadhara

Komredi Kinana akikaidhiwa kadi ya Chadema na aliyekuwa Katibu Mwenezi wa  chama hicho Wilaya ya Rombo na Katibu wa Mbunge wa Chadema wa Jimbo la Rombo, Joseph Selasini, John Tarimo, baada ya kutangaza kukihama chama hicho na kujiunga na CCM wakati wa mkutano huo uliofanyika mjini Tarakea.

KLatika mkutano huo watu wengi wa vyama vya upinzani walikabidhi kadi zao kwa Komredi kwa lengo la kujiunga na CCM.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.