KOMREDI KINANA AMALIZA ZIARA KWA KISHINDO MKOANI ARUSHA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkuutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha wakati wa kuhitimisha ziara katika Mkoa wa Arusha ambayo ilikuwa na lengo la kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Komredi Kinana ambaye katika ziara yake ameambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ametumia Km 2671 kuzungunka katika majimbo 7 ya mkoa huo,  ambapo amefanya mikutano 69 na kukagua miradi ya maendeleo 7 na kuvuna wanachama wapya 4740 miongoni mwao wakiwemo  519 kutoka upinzani.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisisitiza jambo katika mkutano huo ambapo kwa kiasi kikubwa alielezea mafanikio makubwa ya ziara hizo katika mikoa 28  nchini.
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Hasna Mwilima, akicheza ngoma ya kikundi cha Wastara.
 Mbunge wa Viti Maalum kupitia Vijana, Catherine Magige akihutubia katika mkutano huo
 Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Arusha, akihutubia katika mkutano huo
 Komredi Kinana akipokea zawadi ya ngao iliyotolewa na Umoja wa Vijana wa Mkoa wa Arusha , kwa kumpongeza kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi.
 Komredi Kinana akipokea kadi kutoka kwa wanachama wapya kutoka upinzani
 Aliyekuwa Katibu Mwenzi wa Chadema Kata la Orolien Prosper Mfinanga akivua magwanda ya chama hicho baada ya kujiunga na CCM
 Mfinanga (kulia0 akishangilia baada ya kuvua magwanda huku akiungwa mkono na Nape pamoja na Kada wa CCM
 Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Monduli, Amani Silanga akionesha fulana ya chama hicho na baadaye kuamua kuitupa ikiwa ni ishara ya kuachana kabisa na CHADEMA NA KUJIUNGA NA ccm
 Silanga akipiga magoti kuomba msamaha kwa wananchi kwa makosa yote aliyoyafanya akiwa Chadema.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Onesmo Nangole akizungumza katika mkutano wa hadhara jijini Arusha, na kuwataka mawaziri akiwemo Waziri Mkuu kuiga mfano wa Kinana na Nape wa kwenda kuwatembelea wananchi kusikiliza kero zao na kuzitatua badala ya kukaa maofisini
 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano huo na kusisitiza kwamba atahakikisha CCM itarudi kwenye hadhi yake ya awali kama ilivyokuwa wakati wa Baba wa Taifa, Julius Nyerere.

 Wananchi wakimshangilia Komredi Kinana alipokuwa akiondoka baada ya mkutano kumalizika


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*