MAMA MARIA NYERERE AKANUSHA UVUMI ULIOENEA KUWA AMEFARIKI DUNIA


unnamed (69)
Kwa hisani ya http://issamichuzi.blogspot.com/
Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere leo amezungumza na waandishi wa habari,nyumbani kwake Msasani jijini dar es salaam juu ya uvumi ulioenea nchini kuwa amefariki Dunia.Mama Maria amewathibitishia watanzania kuwa bado yu hai na mwenye nguvu hivyo wasiwe na hofu nae.Alisema jana amepokea simu nyingi sana kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo watoto zake, wake wa watoto zake wote, familia yake pamoja na watu mbalimbali ili kumjulia hali.

Amesema alipopokea taarifa hizo wala hakushtushwa badala yake alifanya sara kwani uvumi huo wawezekana inatokana na vuguvugu la uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu, pia utandawazi uliopo wa sayansi na teknolojia wa karne ya 21.
“jana nilipokea simu nyingi sana kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo watoto wangu, wake wa watoto zangu, pamoja na familia,walikuwa wakinisalimia, wengine waliposikia sauti yangu walikata simu” alisema Mama Maria.
Mama Maria alisema taarifa hizi za kuzushiwa kifo si mara ya kwanza kwani hata miaka ya nyuma akiwa na hayati baba wa Taifa, mwalimu Julius Nyerere walipokea taarifa nyingi za uvumi wa kifo.
Mjane wa hayati Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) nyumbani kwake Msasani jijini dar es salaam leo,juu ya uvumi wa kufariki Dunia ulioenea jana kupitia simu na mitandao ya kijamii.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.