MCT YAIPONGEZA TANZANIA BLOGGERS NETWORK (TBN), YAAHIDI KUSHIRIKIANA NAYO

Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani. Baadhi ya bloggers wakipiga picha ya ukumbusho na mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mkajanga (wa tano kulia) katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyokutanisha bloggers kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani.[/caption] [caption id="attachment_55607" align="aligncenter" width="800"]Mkongwe kwa maswala ya kublog hapa nchini, Muhidin Issa Michuzi (wa kwanza kulia) akifafanua jambo kwa baadhi ya wageni waalikwa juu ya kukutana kwao kwenye hafla hilo iliyofanyika juzi Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Mkongwe kwa maswala ya kublog hapa nchini, Muhidin Issa Michuzi (wa kwanza kulia) akifafanua jambo kwa baadhi ya wageni waalikwa juu ya kukutana kwao kwenye hafla hilo iliyofanyika juzi Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_55606" align="aligncenter" width="800"]Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Simu ya Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa ambao ndio walikuwa wadhamini wakuu wa hafla ya TBN, akizungumza machache katika hafla hiyo. Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Simu ya Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa ambao ndio walikuwa wadhamini wakuu wa hafla ya TBN, akizungumza machache katika hafla hiyo.[/caption] [caption id="attachment_55612" align="aligncenter" width="800"]Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Joachim Mushi (kushoto) akimkabidhi mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mkajanga moja ya dhawadi zilizotolewa na baadhi ya wadhamini wa hafla ya TBN. Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Joachim Mushi (kushoto) akimkabidhi mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mkajanga moja ya dhawadi zilizotolewa na baadhi ya wadhamini wa hafla ya TBN.[/caption] [caption id="attachment_55609" align="aligncenter" width="800"]Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani. Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani.[/caption] [caption id="attachment_55610" align="aligncenter" width="800"]Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani. Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani.[/caption] [caption id="attachment_55611" align="aligncenter" width="800"]Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani. Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani.[/caption] [caption id="attachment_55613" align="aligncenter" width="800"]Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani. Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani.

 BARAZA la Habari Tanzania (MCT) limekubali kuanza ushirikiano na uhusiano mzuri na Chama cha Bloggers Tanzania (TBN) mara kitakapo maliza mchakato wa usajili wake na kutambulika rasmi kisheria. MCT imesema kwa hatua ya kwanza itafanya mazungumzo na viongozi wa TBN na kujadiliana namna gani ya kuisaidia TBN.

 Kauli hiyo imetolewa juzi jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mkajanga alipokuwa akizindiwa hafla ya kwanza ya mwaka 2015 ya wamiliki na waendeshaji wa blogu na mitandao mingine
ya kijamii iliyofanyika katika Hoteli ya Serena.

 Katibu huyo Mtendaji wa MCT alisema kwa maendeleo ya sasa ya teknolijia ya habari na mawasiliano ni vigumu kuzitenga blogu kama vyombo vya habari, hivyo kuahidi kushirikiana na TBN kuhakikisha inafikia malengo yake ya kuwaunganisha bloggers na kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili.

 Alisema MCT inasubiri TBN ipate usajili kisheria toka mamlaka husika serikalini na baada ya zoezi hilo itaanza kushirikiana maramoja na chombo hicho kilichoanzishwa kuwaunganisha wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya kijamii nchini na wale wanaofanya shughuli za nje ya nchi. "..

.MCT ipo tayari wakati wowote kuanza kushirikiana nanyi kikazi, tunachosubiri ni TBN kusajiliwa rasmi...mtakapo maliza usajili tu njooni ofisi, tutazungumza na viongozi wenu ili kujua nini cha kuwasaidia. Naombeni msichelewe tuanze hili mara moja," alisema Kajubi Mkajanga akizungumza na wana-TBN kabla ya kuzinduwa sherehe hiyo. Awali akizungumza katika hafla hiyo Mwenyekiti wa TBN,


 Joachim Mushi alisema kwa sasa mitandao ya kijamii imekuwa ikitekemewa na kundi kubwa la jamii katika kusambaza taarifa kwa haraka licha ya uwepo wa changamoto kadhaa ndani ya tasnia hiyo.

 Alisema pamoja na mambo mengine, TBN imeanzishwa kwa lengo la kuwaunganisha waendeshaji na wamiliki wa blogu pamoja na mitandao mingine ya kijamii, na pia kuhakikisha wana-TBN wanapata fursa ya kujifunza zaidi maadili ya tasnia ya habari na mawasiliano ili kufanya kazi zao kiufanisi zaidi.

 Aidha aliishukuru Kampuni ya Simu ya Vodacom Tanzania kwa kusaidia kufanikisha tukio la kukutana 'bloggers', pamoja na Benki ya NMB na makampuni mengine ya Coca Cola, AIM Group na kampuni ya huduma za intanenti ya Raha kufanikisha tukio hilo la kuwaleta pamoja bloggers wa Tanzania.

 Akisoma risala ya wana-TBN kwa mgeni rasmi, Mjumbe wa TBN, Henry Mdimu alisema licha ya blogu kuwa chanzo kikubwa cha habari na mstari wa mbele kuwafikishia wananchi habari kwa haraka zaidi lakini bado zimekuwa hazitambuliwi na mamlaka zinazosimamia na kutetea tasnia nzima ya habari. "...Pamoja na kazi kubwa na nzuri inayofanywa na 'bloggers' na waendeshaji wa mitandao ya kijamii, bado hawatambuliki rasmi na mamlaka husika pamoja na taasisi zinazohusika na usimamizi wa tasnia hii likiwemo Baraza la Habari Tanzania (MCT), Idara ya Habari (Maelezo),

MISA-Tan na hata Mfuko wa Ruzuku kwa Vyombo vya Habari nchini (TMF). "..Tunasema hivi maana tunaona kwa namna moja ama ingine wadau hawa muhimu hawajumuishwi katika harakati au michakato yoyote ile mnayoifanya kwenye tasnia hii. Mfano kupata semina za MCT, kupewa vitambulisho (Press card), kushiriki katika mafunzo na hata mashindano ya kila mwaka ya wanahabari yanayoandaliwa na MCT," alisema Mdimu akisoma risala ya TBN mbele ya mgeni rasmi Bw. Mkajanga.

 Kwa upande wa waalikwa rasmi kutoka ubalozi wa Marekani wakizungumza katika hafla hiyo kupitia kwa mwakilishi wao ameahidi kuisaidia TBN katika programu mbalimbali ili kuchochea uhuru wa habari nchini Tanzania. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.