MKUU WA WILAYA KINONDONI PAUL MAKONDA AKUTANA NA WANA UMOJA WA MAFUNDI MAGARI TEGETA KUTATUA MGOGORO WA ARDHI DHIDI YA MWEKEZAJI
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akiwa na Viongozi wa
Umoja wa Mafundi Magari Tegeta wakati akikagua eneo lenye mgogoro wa
ardhi kati ya wanaumoja huo pamoja na mwekezaji alipokwenda kuwasikiliza
kuhusu mgogoro huo Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akiwa na viongozi wa umoja huo.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja huo Nationi Ndela akitoa historia ya mgogoro huo mbele ya DC Makonda.
Baadhi ya mafundi magari katika gereji za Tegeta wakimsikiliza DC Makonda wakati akiwahutubia ili kupata muafaka wa mgogoro huo.
Baadhi ya gereji zilizopo katika eneo hilo la mgogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda (katikati), akijaribu moja ya mashine ya kuchonga vyuma iliyopo katika eneo hilo.
Baadhi ya mafundi na wamiliki wa gereji mbalimbali katika eneo hilo la mgogoro wakimsikiliza DC Makonda.
Wanaumoja hao wakiwa kwenye mkutano huo.
Hapa DC Paul Makonda akizungumza na wananchi wa Bunju B Kitunda ambao nao wanamgogoro na mwekezaji katika eneo hilo.
…………………………………………………………………………………..
Dotto MwaibaleMKUU
wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda ameanza kufanya juhudu za makusudi
za kujaribu kumaliza mgogoro wa ardhi kati ya Umoja wa Mafundi Magari
Tegeta dhidi ya mmoja wa wawekezaji wilayani humo.Jitihada
hizo ameanza kuzichukua ili kujaribu kumaliza mgogoro huo uliodumu kwa
muda mrefu na kudumaza shughuli za maendeleo katika eneo hilo la mgogoro
lililopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza
Dar es Salaam jana na mafundi eneo la Tegeta zilipo gereji mbalimbali
zinazo milikiwa na wanaumoja hao alitoa mapendekezo ya kukutana na
viongozi wa umoja na mwekezaji ili kufanya mazungumzo ya pamoja kwa
ajili ya kutafuta muafaka wa mgogoro huo.
“Eneo
hili tayari mahakama imemtambuwa mmiliki wake ambaye ndio mlalamikaji
lakini hata hivyo kuna kila sababu ya kukutana na pande zote pamoja na
mwekezaji huyo ili tupate ufumbuzi wa mgogoro huu ili uishe ili shughuli
za maendeleo ziweze kuendelea” alisema Makonda.
Akizungumzia
mgogo huo Naibu Katibu mku wa umoja huo Nationi Ndela alisema ni wa
siku nyingi na kuwa kila wanapokwenda wamekuwa hawafanikiwi ambapo
walimuomba mkuu huyo wa wilaya kuwasaidia.
Ndela
alisema uwekezaji waliouweka katika eneo hilo unafikia zaidi ya
sh.bilioni 35 hivyo ni vizuri serikali ikaliangalia jambo hilo kwa ajili
ya kutoa kipaumbele kwa wawekezaji wa ndani.
Alisema
kwamba mwekezaji anayedaiwa kumiliki eneo hilo alikuwa na kiwanda cha
kutengeneza mabati aina ya asbesto na mara ya mwisho kufanya uzarishaji
wa bati hizo ilikuwa kwenye miaka ya 70 tangu wakati huo eneo hilo
lilikuwa wazi.
DC
Makonda mbali ya kukutana na wamiliki wa gereji hizo pia alikutana na
wananchi wa Bunju B Kitunda ambao nao wanamgogoro wa ardhi na mwekezaji
ambapo aliwataka viongozi wa eneo hilo kufika ofisini kwake baada ya
sikukuu ya pasaka ili kujua chanzo cha mgogoro huo.
Makonda
ilikukabiliana na migogoro ya ardhi katika wilaya yake ameanzisha
utaratibu wa kukutana na pande zinazovutana kila Ijumaa ili kuitafutia
muafaka.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
Comments