MSAMA AKABIDHI MILIONI MBILI KWA AJILI KUSIDIA MAPAMBANO DHIDI YA MAUAJI YA ALBINO


 Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama akimkabidhi fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni moja Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa ya Chama cha Albino Tanzania, Mohamed Chanzi kwa ajili kuunga mkono kampeni ya kupinga mauaji ya albino. Kushoto ni Mweka Hazina wa Chama hicho, Abdilah Omari na wa pili kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha la Pasaka, Hudson Kamoga. Mbali na fedha hizo Msama alikabidhi hundi ya sh. milioni moja. (Picha na Francis Dande)
  Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama akimkabidhi fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni moja Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa ya Chama cha Albino Tanzania, Mohamed Chanzi kwa ajili kuunga mkono kampeni ya kupinga mauaji ya albino. Katika ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha la Pasaka, Hudson Kamoga. Mbali na fedha hizo Msama pia alikabidhi hundi ya sh. milioni moja. 
 Msama akikabidhi hundi ya sh. milioni moja kwa Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa ya Chama cha Albino Tanzania, Mohamed Chanzi. Katikati anayeshuhudia ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha la Pasaka, Hudson Kamoga. 
 Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msamaakifafanua jambo.
Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa ya Chama cha Albino Tanzania, Mohamed Chanzi akitoa neno la shukrani.

Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha la Pasaka, Hudson Kamoga.

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Msama Promotions, waandaaji wa Tamasha la Pasaka, kupitia kitengo chake cha maafa, imetoa msaada wa sh. milioni 2 kuunga mkono kampeni ya kupinga mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini (albino).

Akitoa hundi ya fedha hizo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama, alisema anaungana na Rais Jakaya Kikwete katika hatua ya kupinga ukatili na mauaji ya albino.

Alisema fedha hizo zitatumika kuongeza nguvu ya kuhamasisha juhudi za kupinga vitendo vya kikatili dhidi ya albino, kwani na wao ni binadamu kama walivyo watu wengine.

“Nawaomba wadau na Watanzania kwa ujumla, wazidi kuunga mkono harakati hizi ili kukomesha mauaji yanayoendelea nchini pamoja na kutoa elimu kwa watu wenye dhana potofu ya kuamini kwamba viungo vya albino vinatajirisha,” alisema.

Pia Msama aliiomba serikali itenge eneo maalumu lenye ulinzi mkali ili kuwaweka watoto albino, ambao hawana uwezo wa kujilinda dhidi ya vitendo wanavyofanyiwa.

Naye Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Albino Tanzania (TAS), Mohammed Chanzi, aliishukuru kampuni hiyo kwa kugundua umuhimu wa kulinda watu wenye ualbino nchini.
“Hatuna pa kukimbilia zaidi ya kumuomba Mungu na wadau mbalimbali kutusaidia, kwani hata sisi tunatamani kuishi kama binaadamu wengine, pia tunaomba taasisi na Watanzania wasikie kilio chetu na kutuunga mkono katika hili,” alisema.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI