VIJANA mkoani Mbeya wametakiwa
kutumia gharama za aina yoyote ili kulinda umoja, usalama na amani ya Mkoa
pamoja na taifa kwa ujumla kwa kuepuka vitendo vinavyoweza kuashiria machafuko.
Hayo yalibainishwa na
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) Mkoa wa Mbeya,Amani
Kajuna, alipokuwa akizungumza na wananchi pamoja na wachezaji katika fainali ya
ligi ya mpira wa miguu ya Tarafa ya Tembela iliyofanyika jana katika kiwanja
cha shule ya Msingi Iwalanje wilaya ya Mbeya.
Kajuna alisema ikiwa vijana
hawatajitoa kuwa wazalendo kwa nchi yao pindi machafuko yatakapotokea
watakapokimbilia mipakani mwa nchi walizopakana nazi majina yatabalidilishwa na
kuitwa wakimbizi.
Alisema ili kuepuka kuitwa
wakimbizi ni lazima vijana ambao ni wengi katika taifa wakajitoa kwa gharama
yoyote kulinda amani na utulivu uliopo ikiwa ni pamoja na kuwaogopa wanasiasa
kuwadanganya na kuwashawishi kuingia kwenye tabia hatarishi.
Aidha Kajuna alitumia muda huo
kuwasihi vijana kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha kwenye daftari la
kudumu la wapiga kura ikiwa ni pamoja na kuipigia kura katiba inayopendekezwa.
Awali katika mchezi huo wa
fainali ambao ulizikutanisha timu za Inyala fc na Iwalanje zote kutoka Tarafa
ya Tembela ambapo timu ya Inyala ilishinda kwa changamoto ya mikwaju ya penati
6 dhidi ya penati 5 za Iwalanje fc.
Timu hizo zililazimika
kupigiana mikwaju ya penati baada ya dakika tisini za muda wa kawaida kuisha
kwa bila timu kushindwa kuliona lango la mwenzake.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
kamati ya Mashindano hayo, Yohana Monga, alisema ligi ya Tarafa ilianza Januari
tatu mwaka huu ikishirikisha timu 17 kutoka katika Kata tano za Tarafa ya
Tembela.
Alisema ligi hiyo iliokuwa
imedhaminiwa na Mwenyekiti wa UVCCM, Aman Kajuna ambaye pamoja na gharama za
zawadi kwa washindi alitoa jumla ya shilingi Milioni 1,250,000.
Alizitaja zawadi zilizotolewa
kwa washindi kuwa ni mshindi wa kwanza ambaye ni timu ya Inyala shilingi
300,000. Mshindi wa pili ambaye ni Iwalanje shilingi 200,000, mshindi wa tatu
shilingi 100,000.
Aliongeza kuwa zawadi zingine
zilienda kwa mfungaji bora, mwamuzi bora, mlinga mlango bora na mchezaji bora
ambao kila mmoja alijinyakulia shilingi 50,000 huku Kamati ikipewa shilingi
300,000 pamoja na mchifu wanne ambao kila mmoja alipewa shilingi 20,000/=.
Mwisho.
Comments