NAPE;TUHUMA ZA KUTAKA KUUAWA DK.SLAA NI ZA KIPUUZI



Tarehe 08/03/2015, Dr. Wilbroad Slaa Katibu Mkuu wa Chadema kupitia kwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Ndugu Mabere Marando alitoa tuhuma kwa Serikali na kuwahusisha baadhi ya viongozi wa juu wa CCM kuwa wanapanga njama za kumdhuru Katibu Mkuu huyo wa Chadema.
 
Kimsingi tuhuma hizi ni za kipuuzi, lakini uongo huu usipojibiwa unaweza kugeuzwa kuwa ajenda na Chama hiki cha Chadema kwa kukosa ajenda zingine za maana. Hakuna asiyejua kuwa Chadema kwa sasa kinapumulia mashine, hivyo maneno na matendo yao kwa sasa lazima yalenge kujaribu kujinasua na balaa la kufa kwa chama chao.
Ni vizuri Watanzania wakakumbuka historia ya tuhuma lukuki zilizowahi kutolewa na Katibu Mkuu huyu wa Chadema toka aanze siasa na ambazo zote zilikuja thibitika kuwa ni za uongo. Hapa nitawakumbusha baadhi.
 
Akiwa Singida katika kampeni za Urais za mwaka 2010, Dk. Slaa aliwatangazia wananchi mkutanoni kwamba kulikuwa kumekamatwa lori kubwa la mizigo (semi-trela) lililojazwa karatasi za kura za Urais zilizokuwa tayari amepigiwa kabisa mgombea Urais wa CCM, Dk. Jakaya Kikwete.

Katika kuonyesha kwamba alikuwa na uhakika wa jambo hilo, alisoma hadi namba za lori hilo na tela lake kutoka kwenye karatasi aliyokuwa ameshika mkononi, kisha akasema kuwa lori hilo lilikamatwa katika mji mdogo wa Tunduma, mkoa wa Mbeya wakati likiingia nchini kutoka Lusaka, Zambia.

Lakini baada ya polisi kuchukua hatua za haraka wakitumia namba za lori na tela lake alizokuwa amezisoma na kulikamata, kisha wakalipekua hadharani huku wananchi wakishuhudia palepale Tunduma, kilichokutwa ndani ya lori ilikuwa shehena ya vipodozi vya kina mama na sabuni za manukato.

Baada ya siku chache huku akiwa amesahau yote, Dk. Slaa akatangaza tena kuwa mgombea Urais wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alikesha katika hoteli ya Lakairo, Mwanza akiweka mikakati ya kuiba kura siku ya uchaguzi huo wa mwaka 2010 ili ashinde. Siku chache alisema kura zimeingizwa na zimeshapigwa, hapa amesahau anadai ndio kwanza mpango unapangwa.

Aliwataja watu wengine aliodai walikuwa pamoja na Rais Kikwete kuwa ni aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz na Mkurugenzi wa Hoteli hiyo iliyopo katika jiji la Mwanza, Lameck Airo. Lakini wakati Dk. Slaa akisema uongo huo, Rais Kikwete siku nzima na usiku wake wote alikuwa Mtwara akiendelea na kampeni zake za Urais.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.