Rais Kikwete akutana na Rais Uhuru Kenyatta mjini Windhoek, Alhaj Mwinyi na Mzee Mkapa waungana naye sherehe za kuapishwa rais mpya wa namibia

 .Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya jijini Windhoek Namibia ambapo walihudhuria sherehe za kuapishwa Rais mpya wa Namibia.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake akikutana na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya katika Hoteli ya Safari Court jijini Windhoek Namibia jana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi(kulia) na Benjamin William Mkapa(kushoto) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hosea Kutako jijini Windhoek Namibia leo.Viongozi hao walihudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 25 ya Uhuru wa Namibia ambapo pia Rais wa awamu ya tatu  wa Namibia Dkt.Hage Geingob aliapishwa katika uwanja wa Independence jijini Windhoek.Chama cha ukombozi cha Namibia SWAPO kilizaliwa nchini Tanzania na kuendesha harakati za ukombozi mpaka mwaka 1990 ambapo nchi hiyo ilipata uhuru. Picha na Freddy Maro.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI