SAKATA LA JARIBIO LA KUUAWA, DR. SLAA LATINGA KITUO CHA POLISI


Gari la Dr. Slaa likiwa limepaki nje ya Kituo cha Polisi Central.
Waandishi wa habari (kulia) wakimsubiri Slaa nje.
..Slaa(kulia), akitoka katika lango kuu la kituo cha Polisi akiwa na viongozi wengine wa chama hicho.
Akihojiwa na Wanahabari.KATIBU Mkuu wa Chadema, Dr. Willbroad Slaa, ameripoti katika Kituo cha Polisi Central kilichopo Posta jijini Dar kuhusiana na sakata zima la mlinzi wake anayetuhumiwa kutaka kumuua.
Akizungumza na wanahabari kituoni hapo, Slaa alisema yeye hakuitwa na Jeshi la Polisi kujielezea bali kutokana na maneno yanavyozidi kusambaa na kuwasilishwa ndivyo sivyo ameona aende kueleza ukweli ulivyo. 
Alisema kuwa, kwa mujibu wa chama chake, ameona ni vyema kwenda kulieleza Jeshi la Polisi kuhusiana na ishu nzima inayomkabili mlinzi wake, ambapo alikutana na Kamanda wa Kanda Maalum Mkoa wa Dar es Salaam, Suleimani Kova na kumueleza kila kitu kwa kuandika karatasi tisa (9) zenye maelezo yake, hivyo zoezi zima la kutoa taarifa kuhusiana na alichoandika ameliachia Jeshi la Polisi baada ya wao kufanya kazi yao ya Uchunguzi.
“Ndugu zangu wanahabari sijaitwa hapa kwa ajili ya mahojiano kama taarifa zinavyozaga lakini kutokana na uongozi nilionao nimeona ni vyema suala hili nilifikishe Polisi, na katika maelezo yangu nimeweza kuandika zaidi ya karatasi tisa (9) zenye ukweli mtupu, hivyo nimelikabidhi Jeshi la Polisi na baada ya wao kufanya uchunguzi litatoa taarifa kamili juu ya kile nilicho kiandika,’’ alisema Dr. Slaa. 

(PICHA/STORI NA DENIS MTIMA/GPL)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI